Na wafanyakazi wa Sabahi
Waandishi wa habari kumi na sita wameuliwa hadi sasa mwaka huu kwa
mabomu na watu wenye silaha, jambo linalothibitisha kwa nini watetezi wa
haki za vyombo vya habari, Waandishi wa Habari Wasio na Mipaka (RSF)
wameuita mwaka 2012 kuwa "mwaka wa vifo" katika kumbukumbu za waandishi
wa habari wa Somalia, kupita mwaka 2009 ambapo waandishi tisa
walifariki.
Waombolezaji wakibeba mwili wa mwandishi
wa habari wa Somalia Abdisatar Dahir Sabriye aliyeuawa katika
mashambulio mawili ya kujitoa muhanga kwenye mkahawa hapo tarehe 20
Septemba katikati ya Mogadishu. [Na Mohamed Abdiwahab/AFP]
RSF waliita nchi hivyo baada ya mabomu mawili ya kujitoa muhanga kuua
kiasi cha watu 14, ikiwa ni pamoja na waandishi wa habari watatu hapo
tarehe 20 Septemba. Wiki moja baadaye, waandishi wa habari wawili zaidi
waliuliwa katika mji mkuu.
Wasimamizi wa Haki za Binadamu (HRW) waliitaka serikali mpya ya Somalia
kuagiza ufanyike uchunguzi katika mauaji ya waandishi wa habari.
"Waandishi wa habari wa Somalia wamekuwa kwa muda mrefu wa mwanzo katika
orodha ya walengwa wa pande zote wakati wa vita vya kikatili vya
wenyewe kwa wenyewe," Leslie Lefkow, naibu mkurugenzi wa HRW sehemu ya
Afrika, alisema hapo tarehe 24 Sepetemba. "Rais mpya wa Somalia anaweza
kuchukua hatua za kumaliza mtindo huu wa kutisha kwa kuagiza kufanyika
uchunguzi wa haraka na makini kuhusu mauaji haya."
Hii sio mara ya kwanza kwa RSF kutoa tahadhari juu ya vurugu dhidi ya
waandishi wa habari nchini Somalia. Mwaka 2011, waliita Somalia kuwa ni
taifa la vifo vingi zaidi vya waandishi wa habari barani Afrika, na
kuongeza kuwa tayari waandishi wa habari 25 waliuawa nchini Somalia
kuanzia mwaka 2007 hadi 2011.
Comments