Vurugu kubwa zimezuka kati ya polisi na kundi la Waislamu ambao
walivamia kituo cha polisi maturubai Mbagala kizuiani jijini Dar Es
Salaaam kwa lengo la kushikikiza kupatiwa kijana mmoja ambaye anadaiwa
kukojolea msaafu ili wamuadhibu kwa kitendo hicho.
ENEO la Mbagala Kizuiani, Dar es Salaam jana liligeuka uwanja wa mapambano kati ya makundi ya watu wanaosadikiwa kuwa ni Waislamu na polisi baada ya watu hao kuvamia Kituo cha Polisi Kidogo cha Maturubai kilichopo eneo hilo.
Watu hao walivamia kituo hicho wakitaka wakabidhiwe mtoto anayedaiwa kukojolea kitabu kitakatifu cha Quran ili wamwadhibu.
Vurugu hizo zilizoanza tangu saa nne asubuhi, zilisababisha makanisa matano kuchomwa moto, magari kadhaa kuvunjwa vioo na watu hao.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Temeke, David Misime alisema watu kadhaa wanashikiliwa na polisi kuhusiana na tukio hilo... “Siwezi kutaja idadi ya waliokamatwa, lakini kuna watu tunawashikilia kutokana na kufanya fujo, kwa sasa niko katika operesheni, nitazungumza kwa kirefu baadaye.”
Hata hivyo, Misime alisema hakuna kifo kilichotokea wala majeruhi.
“Pamoja na kwamba bado tupo katika eneo la tukio bado hatujashuhudia vifo wala majeruhi na tunaomba Mungu mambo hayo yasitokee.
Aliyataja makanisa hayo kuwa ni la TAG Kizuiani, Wasabato Kizuiani, TAG la Shimo la Mchanga na KKKT Mbagala Zakheim. Endelea kusoma Gazeti la Mwananchi

Comments