Rais Obama akiwa katika kampeni za urais huko Las Vegas, Nevada October 24, 2012.
Rais wa Marekani Barack Obama anafanya kampeni zake nchi nzima Alhamis
huku mpinzani wake Mitt Romney wa chama cha Republican analenga juhudi
zake za kampeni kwenye jimbo muhimu la Ohio.
Obama amepita kufanya kampeni Alhamis katika majimbo ya Florida,
Virginia, Illinois na Ohio. Huko Illinois atapiga kura yake ya uchaguzi
mkuu wa mwaka huu akizingatia kwamba ni makazi aliyokulia kabla ya
kuingia White House na vile vile jimbo hilo lina sheria iliyopitishwa
kwa kila mtu anayestahiki kupiga kura anaweza kupiga kura yake siku
kadhaa kabla ya siku ya mwisho ya uchaguzi mkuu.
Vituo vingine vitatu ni kwa ajili ya kampeni za kuwahamasisha wapiga kura ambao bado hawajaamua wampigie nani kura katika uchaguzi mkuu wa urais. Anatarajiwa kurudi Washington Alhamisi jioni.
Vituo vingine vitatu ni kwa ajili ya kampeni za kuwahamasisha wapiga kura ambao bado hawajaamua wampigie nani kura katika uchaguzi mkuu wa urais. Anatarajiwa kurudi Washington Alhamisi jioni.
Wakati huo huo bwana Romney ataendelea kuwepo katika jimbo la Ohio
akitembelea miji ya Cincinnati, Worthington na Defiance kwa ajili ya
kufanya mikutano ya kampeni.
Wakati kampeni zikizidi kupamba moto bwana Obama alionekana kwenye
kipindi cha televisheni cha Tonight Show kinachoendeshwa na Jay Leno,
Jumatano akiahidi kutekeleza ahadi zake za kampeni.
Majimbo ambayo bwana Obama na bwana Romney wanayatembelea Alhamis
yatatoa umuhimu wa kuelezea nani atapata kura za wajumbe 270 za wabunge
waliohitajika kumuwezesha mgombea kushinda na kuingia White House.
Comments