Waganda wakusanyika pamoja katika Uwanja
wa Kololo nchini humo, kuadhimisha miaka 50 ya Uhuru wa Uganda kutoka
utawala wa kikoloni wa Uingereza
Hakuna siku ilioonesha umoja wa waganda na mshikamano na kujivunia kuwa
raia wa Uganda kama siku hii ya leo, hivyo ndivyo baadhi ya waganda
wanavyohisi siku ya leo Oktoba 9 mwaka wa 1962, ambapo ni miaka 50 tangu
walipojinyakulia uhuru kutoka kwa utawala wa kikoloni wa Uingereza.
Usalama umeimarishwa katika Sherehe hizo kubwa zinazofanyika Uganda na
kuongozwa na rais wa nchi hiyo, Yoweri Museveni. Sherehe hizo
zinahudhuriwa pia na wakuu wa nchi kadhaa za kiafrika, wakiwemo rais wa
Jamhuri ya Kiemokrasia ya Kongo Joseph Kabila, Rais wa Burundi Pierre
Nkurunzinza, Rais Mwai Kibaki wa Kenya, na Paul Kagame wa Rwanda.
Kulingana na mwandishi wetu mjini Kampala, rais Yoweri Museveni alikuwa
akitarajiwa kuhutubia wananchi ambapo wengi wanaamini kuwa ataeendelea
kusisitiza waganda kuwa na uzalendo.
Kasisi wa kianglikana Luke Orombi ndiye aliyefungua sherehe kwa maombi
akiitakia baraka tele, na kukemea mambo kama ukosefu wa kazi, rushwa,
umaskini na siasa zisizokuwa na muelekeo mzuri katika nchi hiyo.Naye
Mufti wa Uganda, Sheikh Shaban Mubajje aliliombea amani taifa hilo la
Afrika mashariki.
Hata hivyo huku baadhi ya raia wa nchi hiyo wakisherehekea maadhimisho
hayo kuna wale wasioona umuhimu wa miaka hiyo 50 ya Uhuru, wakisema
hakuna chochote cha kujivunia kwa kuwa maskini wanaendelea kuwa maskini
katika taifa hilo lililowahi kutajwa na Waziri mkuu wa zamani wa
Uingereza Winston Churchill kama lulu ya Afrika.
Comments