SIKU zote Waswahili wanasema: “Msemea
sikioni siyo majinuni!” Hata hivyo, ni wachache wanaoweza kuzingatia
yale wanayoambiwa na daima wanapoyafanyia kazi huwa wanapata matokeo
mazuri.
Suala la rushwa ndani ya Chama cha
Mapinduzi limekuwa sugu, wenye fedha wamekuwa wakilangua kura ili kupata
uongozi, hata kama hawana sifa stahiki. Lakini pamoja na ‘Wenye hekima
wa Babeli’ kutahadharisha madhara ya mchezo huo mchafu, bado wahusika
wameziba masikio kwa nta, hawataki kusikia la Muadhini wala Mnadi
Swala!
Matokeo yake CCM limekuwa kokoro kama
alivyopata kusema Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere. Kokoro linalovua
samaki na konokono kwa pamoja, na inahitajika busara na hekima kuweza
kuchambua samaki na konokono hao ambao ni hatari mno.
Uongozi ndani ya CCM ni sawa na
kutangaza zabuni, ambayo mwenye fedha nyingi ndiye anayeshinda na kupewa
uongozi huo. Rushwa imekuwa kansa mbaya ndani ya CCM, fedha zinamwagwa
nje nje na viongozi wao wanaangalia na kuchekelea, wanakemea rushwa na
tabasamu pana kana kwamba ni kitu cha kawaida tu. Hii ni aibu kwa chama
kikongwe na chenye dhamana ya kuongoza Taifa!
Soma zaidi...
www.kwanzajamii.com/?p=4111
Comments