Skip to main content

WFP Na Vodacom Watumia Simu Kubadili Desturi Za Lishe Nchini


Mkurugenzi Mkazi wa WFP nchini Bw.Richard Ragan akiongea na waandishi wa habari (Hawapo pichani) wakati wa utambulisho wa mradi wa majaribio wa uwezeshaji wanawake wajawazito na watoto mkoani Mtwara kupata fedha za kununua chakula chenye lishe. Walengwa watakuwa wakipokea fedha kila mwezi kupitia mtandao wa M-PESA. Kushoto ni Mkuu wa kitengo cha Vodacom Foundation Bw.Yessaya Mwakifulefule.
  Mkuu wa kitengo cha Vodacom Foundation Bw.Yessaya Mwakifulefule (kushoto) akiteta jambo na Mkurugenzi wa WFP nchini Bw.Richard Ragan,wakati wa mkutano na waandishi wa habari kuhusu ushirikiano wa Vodacom Tanzania na WFP katika mradi wa uwezeshaji wanawake wajawazito  fedha za kununulia chakula chenye lihse mkoni Mtwara.  Feha hizo hutumwa kupitia huduma ya M-pesa.

WFP NA VODACOM ZATUMIA TEKNOLOJIA YA SIMU ZA MKONONI KUBADILI
DESTURI ZA LISHE TANZANIA

DAR ES SALAAM – Vodacom Tanzania na Mpango wa Chakula wa Umoja wa Mataifa (WFP) leo
wametangaza ushirikiano ambao utahamasisha jamii zisizokuwa na uhakika wa chakula katika Mkoa wa
Mtwara kupata elimu ya afya na lishe na kwa njia ya kupatiwa msaada wa fedha kupitia mtandao wa
simu za mkononi.

Mradi huu wa majaribio, ambao utazinduliwa Jumanne 9 Oktoba 2012 katika Kata ya Nanguruwe,
Mtwara, utakuza desturi chanya za lishe kwa njia ya kutuma fedha kwa kutumia Vodacom M-Pesa.
Mtwara ni miongoni mwa mikoa yenye tatizo sugu la utapiamlo na ukosekanaji wa virutubishi muhimu
kwa muda mrefu.

Mkurugenzi wa WFP Nchini, bwana Richard Ragan, alisema ushirikiano huo na Vodacom utasaidia
kufikisha elimu ya lishe kwa kaaya zilizolengwa zipatazo 2,200 katika sehemu zote za mkoa wa Mtwara
kwa kutoa motisha kwa kina mama kushiriki kwenye mafunzo.

“Teknolojia ya simu za mkononi ya M-Pesa inatoa njia mbadala ya usambazaji wa chakula,” alisema
Ragan.” Kwa kusaidiana na Vodacom Tanzania, WFP inachangia juhudi za kitaifa za kupambana na lishe
duni hapa Tanzania.”

Akina mama watakaoshiriki watatumiwa kwa M-Pesa kiasi cha TShs 16,000 (takriban dola za
kimarekani 10) kila mwezi , ambazo zitawawezesha kununua chakula kinachojenga afya zaidi na chenye
virutubisho zaidi. Fedha hizi zitatumwa kutegemeana na mahudhurio kwenye kliniki za kuelimisha
kuhusu umuhimu wa lishe kwa mtoto “Katika Siku Zake Elfu Moja za Kwanza ” za maisha ya mtoto,
ikiwa ni pamoja na kumnyonyesha.

Akizungumza kwenye uzinduzi huo, Mkuu wa Vodacom Foundation Bwana Yessaya Mwakifulefule
alisema Vodacom Tanzania itaendelea kuisaidia miradi ya Vodacom Mobile for Good, inayoboresha
maisha ya vikundi vilivyo hatarini hapa nchini kwa kulenga maeneo muhimu ya afya na ustawi wa
jamii.

“Kupitia Vodacom M-Pesa, tutaisaidia WFP kutuma pesa kila mwezi moja kwa moja kwa walengwa
stahili. Hii, pamoja na elimu ya lishe, itawahamasisha akina mama walio wajawazito na wanaolea watoto
wachanga na akina mama wenye watoto walio chini ya miaka 2 kununua chakula kinachojenga afya na

kuifanya milo yao iwe anuwai,” alisema Mwakifulefule.

“Vodacom Tanzania ina furaha kuwa sehemu ya mradi huu kabambe; ni lengo la kampuni kuhakikisha
teknolojia yake ya simu za mkononi inabadili maisha ya watu katika kila sekta nchini,” aliongezea.
Mradi utafanyiwa majaribio katika vijiji 27 katika kata za Nanguruwe, Naumbu, Madimba na Nitekela,
zilizoteuliwa kwa kushauriana na Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara. Huu ni mradi wa kwanza wa
kulipa fedha taslimu ambao WFP iaufanyia majaribio Tanzania, na utapima jinsi malipo ya pesa taslimu
yanavyoweza kufanyika katika miradi ya jamii inayowalenga mama na mwana katika masuala ya, na
shughuli za, lishe.

#

Vodacom Tanzania
Vodacom Tanzania Limited ni kampuni ya simu za mikononi inayoongoza Tanzania inayotoa huduma za
teknolojia ya mawasiliano ya kisasa kabisa ya GSM nchini kote.

Vodacom Tanzania ni kampuni tanzu ya Vodacom Group (Pty) Limited, South Africa, ambayo pia ni
kampuni tanzu ya Vodafone Group UK. Vodacom Group (Pty) Limited ina hisa nyingi zaidi, asilimia 65;
asilimia 35 zilizobaki zinamilikiwa na Mirambo Ltd.

Vodacom Tanzania imetangazwa kuwa Super Brand (Chapa Bora Zaidi) kwa miaka mitatu mfululizo,
kutoka 2009 -2011.

The World Food Programme (WFP)

WFP ni shirika kubwa kuliko yote duniani linalojihusisha na masuala ya kibinadamu na kupiga vita njaa
duniani kote. Kila mwaka, kwa wastani, WFP inawalisha zaidi ya watu 90 milioni katika zaidi ya nchi 70.

Habari zaidi zinapatikana kwenye mitandao ya kijamii: Twitter @wfp_media AND @wfp_africa

Kwa taarifa zaidi wasiliana na:
Fizza Moloo, WFP/Dar es Salaam, Fizza.Moloo@wfp.org Simu. +255 784 720022
Matina Nkurlu, Vodacom Tanzania, mnkurlu@vodacom.co.tz Simu. +255 754 710099

Comments

Popular posts from this blog

MBINU ZA KUMFIKISHA MWANAMKE MWENYE MAKALIO MAKUBWA KILELENI KWA HARAKA

Kwa kawaida wanawake wanafikia kilele (mwisho wa utamu wa ngono) kati ya dakika ishirini na saa moja, yaani kwa kifupi inawachukua muda mrefu sana hali inayopelekea mpenzi mvivu kuchoka na ufanyaji wake utakuwa wa “ovyo” hali itakayo kufanya wewe kuishiwa na hamu ya kuendelea. Pamoja na kuchelewa huko ambako kunatokana na utofauti wetu kati ya mwanaume na mwanamke lakini nakumbuka hapo nyuma nilikutana na wanawake 2 waliokuwa ndani ya ndoa na wamezaa lakini hawajawahi kabisa kujua utamu wa tendo hilo alimaharufu kama “kufanya mapenzi”. Natambua kuwa ni ngumu au niseme si wanawake wote ambao wamejaaliwa kimaumbile kwamba wanafanikiwa kufika kileleni zaidi ya mara mbili kila wanapofanya mapenzi/ngono (kumbuka ni kati ya dakika 15 na saa moja hivyo Jibaba hapa awe na uwezo wa kujizuia kwa zaidi ya dk 45) na ikiwa jamaa ni “mzamiaji” basi unaweza ukaondoka na goli 3 ktk mzunguuko mmoja. Lakini kwa nini basi baadhi yao tu ndio wafike kileleni na wengine was...

Mushikiwabo to UN: Enhance civilian protection

By Eugene Kwibuka Rwanda’s Minister of Foreign Affairs and Cooperation has urged the United Nations Security Council (UNSC) to invest more energy in the prevention of conflicts for better protection of civilians living in conflict-torn areas. Rwanda’s Foreign minister, Louise Mushikiwabo Louise Mushikiwabo made the call during an open debate on the protection of civilians in armed conflict which the UNSC held in New York on Tuesday. “Rwanda’s core message today is that enhancing the protection of civilians in armed conflict requires action before a conflict starts. The proliferation of non-state armed groups makes civilian protection both more urgent, and harder to achieve,” she said. For better protection of civilians in armed-conflict areas, the minister emphasised the need to increase investments in professionalising the military and police forces through adequate training. “Only when the leadership of armed forces shares the international...

Saudi King urges U.N. action against religious insults

Saudi King Abdullah urged the United Nations to produce a resolution condemning insults on monotheistic religions after the anti-Islam film in the U.S. that sparked deadly protests in many Muslim countries last month. (AFP) By AFP, MINA/SAUDI ARABIA Saudi King Abdullah on Saturday demanded a U.N. resolution condemning insults on monotheistic religions after a low-budget film produced in the U.S. sparked deadly protests last month. “I demand a U.N. resolution that condemns any country or group that insults religions and prophets,” he said during a meeting at his palace with religious figures and heads of hajj delegations in the Mina valley where pilgrims were performing final rituals of hajj. “It is our duty and that of every Muslim to protect Islam and defend the prophets.” A low-budget film produced in the U.S., Innocence of Muslims, triggered a wave of deadly anti-American violence last month across the Muslim world targeting US symbols ranging ...