Na Rajab Ramah, Nairobi
Serikali ya Kenya imeweka
miongozo mikali ya kikemea hatuba za chuki wakati nchi inajitayarisha
kufanya uchaguzi mkuu mwezi Machi.
Katibu
Mkuu wa Baraza la maimamu na Wahubiri wa Kenya Sheikh Mohamed Dor
akifikishwa katika mahakama ya Mombasa hapo tarehe 18 Oktoba ambako
alishitakiwa kwa kuchochea vurugu. [Na AFP]
Sheria hizo mpya, zinazoitwa
"Miongozo ya Kuzuia Upelekaji wa Ujumbe wa Siasa Usiotakiwa kupitia
Mitandao ya Mawasiliano ya Elektroniki", zilitangazwa mjini Nairobi siku
ya Jumatano (tarehe 24 Oktoba).
Miongozo hiyo itasimamia ujumbe
zinazotumwa kupitia simu za mikononi pamoja na usambazaji wake katika
mitandao ya kijamii ili kuhakikisha hakuna ujumbe za kuchokoza au
kushawishi unatumwa katika Twitter au Facebook, alisema Katibu Mkuu wa
Wizara ya Habari na Mawasiliano Bitange Ndemo.
Miongozo hiyo inawataka
wanasiasa kupeleka maandiko ya ujumbe wa kampeni zao na matangazo ya
kisiasa kwa ajili ya kuchunguzwa angalau siku mbili kabla haijatumwa,
kusemwa au kutangazwa kwa umma.
Tume ya Taifa ya Maelewano na
Maingiliano, Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka, Tume ya Mawasiliano ya
Kenya (CCK), polisi na sekta nzima ya mawasiliano ya simu, ambazo
zilitoa miongozo hiyo, zitasaidia ili kuimarisha miuongozo hiyo, Ndemo
alisema.
"Wale watakaokiuka kanuni hizi
watapelekwa jela," Ndemo aliiambia Sabahi. Alisema kuwa mtu yeyote
atakayetuma ujumbe za kutishia, kutukana, kunyanyasa na ujumbe za
uchochezi zenye uwezo kuchochea chuki za kikabila kwa kutumia simu za
mikononi na wale wanaovunja sheria za kisiasa watakabiliwa na adhabu ya
faini ya shilingi milioni 1 (dola 11,700), muda wa jela hadi miaka
mitatu, au yote mawili.
Comments