Warembo wanaowania taji la Redd's Miss Tanzania 2012 wakiwa nje ya jengo la Mamlaka ya Hifadhi ya Taifa ya Ngorongoro walikofika kujionea vivutio mbalimbali katika bonde la hifadhi hiyo ambalo lina mambo mengi ya ajabu miongoni mwa hifadhi. Mbali na kujionea wanyama wa aina mbalimbali na ndege pia warembo hao walipata fursa ya kujifunza juu ya Bonde hilo ambalo lipo katika mchakato wa kuingia katika Maajabu ya dunia.
Baadhi ya warembo wanaowania taji la Redd's Miss Tanzania 2012 wakipewa maelezo juu ya picha mbalimbali za Hifadhi ya Bonde la Ngorongoro, wakati warembo hao walipotembelea hifadhi hiyo kwa kujifunza na kujionea mambo mbalimbali. Warembo hao wa Redd's Miss Tanzania 2012 wapo Kanda ya Kaskazini kwa ziara ya kuhamasisha Utalii wa Ndani. Baadhi ya Warembo wa Redd's Miss Tanzania wakiwa pamoja na Watalii wengine wakioangalia maajabu ya Bonde la Ngorongoro ambalo ni moja ya vivutio vinavyotarajiwa kuingia kwenye maajabu ya Dunia.Inatoka kwa mdau.
Comments