Katika utaratibu wa sasa mabilioni ya Rais Kikwete hupitia katika benki
za NMB na CRDB kwa ajili ya kuwakopesha wananchi kupitia vikundi vyao
zikiwemo Vyama vya Kuweka na Kukopa (Saccos).
Akifungua maonyesho ya Vicoba yaliyoandaliwa na Taasisi ya Umoja Aids
Control and Community Youth Development (Uyacode), Lowassa alisema fedha
hizo zikipitia Vicoba utakuwa ukombozi mkubwa kwa wananchi maskini.
Lowassa wamewataka wana–Vicoba kuwashawishi wabunge wao ili walishawishi
Bunge ili fedha hizo ziweze kupitia vicoba vinginevyo wawanyime kura.
“Mbunge ambaye atashindwa kushawishi Bungeni ili mabilioni ya JK yaweze
kwenda moja kwa moja kwa vicoba msimpe kura,” alisema Lowassa.
Alisema wabunge watakaoshindwa kufanya hivyo wasipewe kura kwa sababu
watakuwa wameshindwa kuwasaidia wananchi wao katika kupambana na
umaskini.
Bila kueleza ubaya wa mfumo huo wa sasa wa utoaji wa mabilioni ya JK,
Lowassa alisema yeye ni muumini wa Vicoba anayeamini kwamba unasaidia
wananchi wa kawaida katika kupambana na tatizo la ajira.
Comments