Warembo wanaowania taji la Miss Tanzania 2012 jana walitembelea eneo la Utalii la ufugaji nyoka la mjini Arusha maarufu ARUSHA SNAKE PARK na kujionea nyoka wa aina mbalimbali, Mamba, Kenge, ndege aina ya Bundi, Tai na Tumbiri.
Warembo hao wapo mikoa ya kanda ya kaskazini kwaajili ya kutembelea vivutio mbalimbali vya Utalii nchini na kujifunza mambo tofauti tofauti.
Pamoja na kujionea Nyoka hao na kucheza nao kwa kuwa vaa shingoni pia warembo hao walipata fursa ya kujifunza juu ya tamaduni za Mila ya Wamaasai na kutembelea vibanda vya urembo wa Kimasai.
Comments