Na Othman Khamis Ame
Serikali ya Uholanzi inakusudia kuunga mkono harakati za Kiuchumi na
Maendeleo katika Mpango wake wa kusaidia Mataifa Manane machanga
Ulimwenguni.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi
Seif Ali Iddi akibadilishana mawazo na Balozi wa Uholanzi Nchini
Tanzania Dr. Ad Koek Koek hapo Ofisini kwake Mtaa wa Vuga Mjini
Zabzibar.
Balozi wa Uholanzi Nchini Tanzania Dr. Ad Koek Koek alieleza hayo wakati
alipokuwa akizungumza na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif
Ali Iddi hapo Ofisini kwake Mtaa wa Vuga Mjini Zanzibar.
Balozi Koek Koek alisema Mataifa hayo manane yaliyoko Latin Amerika
pamoja na Afrika Tanzania ikiwa miongoni mwake yanatarajiwa kufaidika na
Mpango utakaohusisha miradi ya pamoja kati ya Makampuni ya Uholanzi na
yale ya Mataifa Washirika.
Aliitaja miradi hiyo kuwa ni pamoja na utengenezaji wa Hospitali Kuu ya
Mnazi Mmoja, Uwanja wa Ndege sambamba na Miundo mbinu ya Bara bara
ambapo utekelezaji wake utaanza mwezi julai mwaka 2013 mara baada ya
kukamilika kwa tathmini pamoja na Bajeti ya Mpango huo.
“Tumependekeza katika kusaidia kunyanyua Uchumi wa Mataifa Rafiki
tumeonelea ni vyema Miradi itakayoanzishwa iwe katika mfumo wa ubia kwa
lengo la kuyapa nguvu za Kiuchumi Makampuni na Taasisi za kizalendo”.
Alifafanua Balozi Koek Koek.
“ Kitu kitakachozingatiwa zaidi katika mpango huo muhimu ni kuhakikisha
wawekezaji wa Makampuni ya pande hizo mbili yanadumisha Ushirikiano wa
karibu zaidi”. Aliendelea kusisitiza Balozi Koek Koek.
Comments