Skip to main content

Tuwe Na Tahadhari Tunapoongelea Muungano-Shivji


MWENYEKITI wa Kigoda cha Mwalimu Profesa Issa Shivji amesema suala la Muungano linapaswa kuangaliwa kwa umakini na kwamba likiachwa kama lilivyo, linaweza kuliingia taifa katika matatizo makubwa.Profesa Shivuji alitoa onyo hilo jana, alipokuwa akizungumza katika mjadala wa Kigoda cha Mwalimu Nyerere, kilichofanyika katika ukumbi wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Mkwawa, mjini Iringa. Kauli hiyo ilikuja baada ya wachangiaji wengi katika mjadala huo kutaka Muungano wa Tanganyika na Zanzibar uvunjwe. “Haya tunayoyajadili ndiyo maneno wanayozungumza wananchi, suala la Muungano lisipuuzwe linapaswa kujadiliwa kwa kina, tusipofanya hivyo madhara yake ni makubwa kwani linaweza kutuingiza kwenye vurugu,”alisema Profesa Shivji. Shivji alionya kuwa suala hilo likiachwa bila kujadiliwa na wananchi wakizuiwa na kutishwa, ili wasijadili Muungano, linaweza kutoa mwanya kwa mataifa yasiyoitakia mema Tanzania kuingia na kuvuruga amani iliyopo. Akuzungumzia haja na umuhimu wa kuajdili Muungano, Profesa Shivuji alisema kwa hali ilivyo sasa, ni muhimu watu kuujadili hasa ikizingatiwa kuwa muungano wa sasa ulihusha viongozi kwa lengo la kulinda maslahi binafsi. Mchokaza mada hiyo, alipendekeza wajumbe kujadili kwa kujibu hoja mbili kuhusu namna ya Muungano wanaoutaka na pia kama mchakato wa kuandika katiba mpya una manufaa kwao. Kuhusu mchakato wa katiba, Profesa Shivji alisema mchakato huo bado unaweza usiwe na matunda kutoka na mafumo muundo wa Bunge maalumu la katiba kutotofautina na ule wa mwaka 1977. Katika mjadala huo, Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai wa Serikali ya Mapinduzi Zanziba, Ibrahim Mzee Ibrahim, aliingia katika malumbano ya kimslahi na mwandishi mkongwe nchini Jenerali Ulimwengu, kila moja akitetea upande wake. Ibrahimu akizungumza katika mjadala huo alisema kuna ripoti inayoonyesha kuwa maslahi yatokanayo na Muungano ni makubwa kuliko matumizi yake lakini hadi sasa hakuna akaunti ya pamoja iliyoundwa kwa ajili ya kuweka fedha hizo. “Ingawa katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 imesema wazi kuhusu kuundwa kwa mfuko wa pamoja na kuwe na akaunti ya kuweka fedha zatokanazo na Muungano lakini hadi leo hakuna kitu hicho, kuna ripoti inaonyesha kuwa mapato yatokanayo na Muungano ni mkubwa kuliko matumizi lakini upande wa bara unakataa kusomwa kwa ripoti hiyo,”alisema Mzee. Mzee alifafanua kuwa ukiachilia mbali tatizo hilo la kiuchumi, pia kuna tatizo la muundo wa Bunge la kupitisha katiba mpya aliodai halijatofautina na mabunge ya namna hiyo yaliyotengeza katiba zilizopita ikiwamo ya mwaka 1977 inayotumika sasa. Kwa upande wake, Ulimwengu alikubalina na Mzee juu ya kuwapo kwa fedha katika Serikali ya Muungano, lakini alitetea kuwa bara haiinyonyi Zanzibar. Katika mjadala huo, Ulimwengu alipendekeza watanzania kuendelea na mjadala juu ya Muungano lengo likiwa kushinikiza viongozi kukubaliana na aina ya muungano wanaotaka. “Mimi sisemi muungano uvunjwe,kama mpangilio utakuwa mzuri wananchi wa Tanganyika na Zanzibar ni ndugu na wanaweza kunufaika na muungano huo, lakini kama juhudi zote za kuboreha Muunngano zitashindikana basi kama walivyosema uvunjwe itabidi iwe hivyo,”alisema Ulimwengu 
Chanzo Mwananchi.Inatokakwa Mjengwa.

Comments

Popular posts from this blog

Thousands of protesters clash with police in Chicago: Chaos in the Windy City as 45 activists arrested and one cop stabbed after demonstrators target NATO

By DAILY MAIL REPORTER Thousands of demonstrators upset with the war in Afghanistan, climate change and the erosion of union rights have raised the intensity of a march in downtown Chicago on Sunday as world leaders assembled for a NATO summit. The protest, one of the city's largest in years, turned violent at the end of an anti-NATO march, where demonstrators confronted Chicago police, pushing against a line of officers several blocks from the lakefront convention center where President Obama hosted a gathering of world leaders. Authorities were seen making arrests one by one and leading individual demonstrators away in handcuffs. After a clash near McCormick Place, Chicago Police Superintendent Garry McCarthy said at a news conference that the protests resulted in 45 people being arrested and four officers suffering injuries - one from a stab wound in the leg. Scroll down for video Clash: Demonstrators try to flee the police as they are move in on them ...

MBINU ZA KUMFIKISHA MWANAMKE MWENYE MAKALIO MAKUBWA KILELENI KWA HARAKA

Kwa kawaida wanawake wanafikia kilele (mwisho wa utamu wa ngono) kati ya dakika ishirini na saa moja, yaani kwa kifupi inawachukua muda mrefu sana hali inayopelekea mpenzi mvivu kuchoka na ufanyaji wake utakuwa wa “ovyo” hali itakayo kufanya wewe kuishiwa na hamu ya kuendelea. Pamoja na kuchelewa huko ambako kunatokana na utofauti wetu kati ya mwanaume na mwanamke lakini nakumbuka hapo nyuma nilikutana na wanawake 2 waliokuwa ndani ya ndoa na wamezaa lakini hawajawahi kabisa kujua utamu wa tendo hilo alimaharufu kama “kufanya mapenzi”. Natambua kuwa ni ngumu au niseme si wanawake wote ambao wamejaaliwa kimaumbile kwamba wanafanikiwa kufika kileleni zaidi ya mara mbili kila wanapofanya mapenzi/ngono (kumbuka ni kati ya dakika 15 na saa moja hivyo Jibaba hapa awe na uwezo wa kujizuia kwa zaidi ya dk 45) na ikiwa jamaa ni “mzamiaji” basi unaweza ukaondoka na goli 3 ktk mzunguuko mmoja. Lakini kwa nini basi baadhi yao tu ndio wafike kileleni na wengine was...

LEO NI BUNGE LA BAJETI

Waziri wa Fedha na Uchumi, Mustafa Mkulo. -WANANCHI WATAKA IPUNGUZE UKALI WA MAISHA MACHO na masikio ya mamilioni ya Watanzania na wadau wa nje, leo yanaelekezwa Dodoma ambako Bajeti ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2011/12 itasomwa.Wananchi wengi wamekuwa na shauku ya kujua mwelekeo wa bajeti hiyo hasa katika kipindi hiki ambacho wanakabiliwa na hali ngumu ya maisha iliyotokana na kupanda kwa bei vyakula na bidhaa za mafuta. Kwa takriban wiki nzima iliyopita, baadhi ya wananchi wamekuwa wakituma ujumbe mfupi wa maandishi kwa simu katika vyombo vya habari, wakiisihi serikali kuhakikisha kuwa bajeti ya mwaka huu inawaondoa katika hali ngumu ya maisha. Bajeti hiyo itakayosomwa bungeni na Waziri wa Fedha na Uchumi, Mustafa Mkulo itatangazwa kwa wakati mmoja na bajeti za serikali za nchi zote za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), katika mtazamo wa kuimarisha mshimakano na umoja wa nchi hizo. Kwa kawaida na mazoea ya muda mrefu, baj...