NA FURAHA OMARY
UPELELEZI wa kesi ya mauaji inayomkabili msanii wa filamu Elizabeth Michael 'Lulu', haujakamilika.
Lulu anayekabiliwa na kesi ya mauaji ya msanii mwenzake, Steven Kanumba, alipanda kizimbani jana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.
Msanii huyo alipanda kizimbani mbele ya Hakimu Mkazi Agustina Mbando, anayesikiliza shauri hilo.
Wakili wa Serikali Mwandamizi Tumaini Kweka alidai shauri hilo linakuja kwa kutajwa na kwamba upelelezi haujakamilika.
Kweka aliiomba mahakama kuahirisha shauri hilo hadi tarehe nyingine. Hakimu Agustina aliahirisha shauri hilo hadi Oktoba 24, mwaka huu. Lulu alirudishwarumande hadi tarehe hiyo.
Lulu anadaiwa kuwa Aprili 7, 2012, saa saba usiku, maeneo ya Sinza Vatican, Dar es Salaam, alimuua Kanumba.
Comments