Skip to main content

Posts

Showing posts from June, 2012

Ngoma Africa Band ndani AFRO-Ruhr Festival !

Mjini Dortmund, Ujerumani jumamosi 30 Juni 2012   Kikosi kazi cha Ngoma Africa Band aka FFU yenye makao yake kule Ujerumani,wanategemewa kukwea jukwaa la Afro-Ruhr Festival, siku ya jumamosi 30 Juni 2012 mjini Dortmund,Ujerumani. Bendi hiyo maarufu ya muziki wa dansi barani ulaya inayoongozwa na mwanamuziki Ebrahim Makunja aka kamanda Ras Makunja wa FFU,itapeleka mzimu wake wote wa dansi katika onyesho hilo kubwa la aina yake,washabiki wa muziki katika onyesho hilo wanakumbana "Jino kwa Jino" na makombora ya muziki wa Ngoma Africa band aka FFU, bendi hiyo kwa sasa inatamba nyimbo zake za "Supu ya Mawe" ,"Uhuru wa Habari" na "Bongo Tambarare" ambazo ipo katika CD ya "BONGO TAMBARARE" pia zinasikika katika kambi yao FFU at www.ngoma-africa.com au http://www.ngoma-africa.com

Annan aelezea matumaini juu ya mkutano wa Syria

Annan aelezea matumaini juu ya mkutano wa Syria Juhudi za kidiplomasia zinaendelea kujaribu kuuokoa mpango wa amani wa Syria siku moja kabla ya mkutano mwingine wa kimataifa ambao unaandaliwa mjini Geneva kutafuta suluhu ya mgogoro uliodumu kwa miezi 16 nchini Syria. Kikwazo kikubwa kwa mkutano huo ni msimamo wa Urusi kusisitiza mabadiliko yafanywe katika mpango wa Kofi Annan, ambao unataka kuundwa kwa serikali ya umoja wa kitaifa nchini Syria, ambayo itashirikisha wajumbe kutoka upande wa serikali na ule wa waasi. Hata hivyo mpango huo uneeleza kuwa wajumbe watakaokubaliwa kutoka upande wa serikali, ni wale ambao kushiriki kwao hakuwezi kukwamisha mchakato wa kuleta utengamano na maridhiano. Wanadiplomasia kutoka nchi za magharibi, wamemueleza Kofi Annan kuwa mkutano huo wa Jumamosi mjini Geneva hautakuwa na maana yoyote, hadi pale maafikiano yatakapofikiwa baina ya waziri wa mambo ya nchi za nje wa Marekani Hillary Clinton na mwenzake wa Urusi...

Qirbi says Yemeni forces regained control of al-Qaeda strongholds

Yemen’s Foreign Minister Abubakr al-Qirbi said his government would need to track down the sources of funding, identify Islamic clerics who propagated extremist views and create jobs for the country's young population. (AFP) By AL ARABIYA WITH REUTERS The Yemeni forces were able to regain control of al-Qaeda’s strongholds in southern Yemen and other regions, Yemen’s Foreign Minister Abubakr al-Qirbi told Al Arabiya on Thursday. “The Yemeni police and army forces were able to kick al-Qaeda militants from the regions that they used to control. They have fled to some mountainous areas,” he Qirbi said. “It is not over yet. Our forces will continue to chase those operatives,” he told Al Arabiya on the sidelines of an anti-piracy conference in Dubai. Meanwhile, he told Reuters in separate statements that some al-Qaeda-linked militants may have fled to neighboring states, including Oman, after being driven out of their strongholds in cit...

WB gives Tanzania 45bn/- to improve UCAF services

By CHRISTOPHER MAJALIWA The government has obtained 45bn/- from World Bank to facilitate Universal Communication Access Fund (UCAF), the House was told on Friday. The Deputy Minister for Communication, Science and Technology, Mr January Makamba UCAF was introduced to subsidize telecommunication companies in course of providing services in areas which were considered to have less business activities. The Deputy Minister for Communication, Science and Technology Mr January Makamba said that there were some areas in the country with limited telecom services due to the fact that the companies were profit-oriented, thus before supplying the service they had to be satisfied with market stability. However, he said that the government having seen how important it was to provide the services to all the people, did all it could to liaise with telecom companies through UCAF to ensure that all areas across the country were supplied with the services...

WEMA AMPA ZAWADI OMOTOLA

Mcheza filamu wa kimataifa wa Nigeria, Omotola Jalade akijaribu kuvaa kanga aliyozawadiwa na mwenyeji wake, msanii nyota wa fani hiyo nchini, Wema Sepetu. Msanii nyota wa filamu nchini, Wema Sepetu akimkabidhi zawadi ya kanga, viatu na shanga, mcheza filamu wa kimataifa wa Nigeria, Omotola Jalade muda mfupi kabla hajapanda ndege na kurejea kwao Nigeria juzi usiku. Kushoto ni Mkurugenzi wa Kampuni ya One Touch Solutions, Petter Mwendapole na katikati ni mwigizaji, Snura. Inatoka kwa mudau.

Taswira Mbalimbali za Waziri Mkuu Mizengo Pinda Bungeni Mjini Dodoma

 Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na  Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Christopher Chiza kwenye viwanja vya bunge Mjini Dodoma  Juni 26, 2012  Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Mbunge wa Moshi Mjini Philemon Ndesamburo (kushoto ) na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Leonidas Gama kwenye viwanja vya Bunge Mjini Dodoma Juni Juni 26,2012. Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Mbunge wa Viti Maalum, Riziki Lulida (katikati) na Mbunge wa Mchinga,Said Mtanda kwenye viwanja vya Bunge Mjini Dodoma Juni 26,2012.Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu

NOKIA 1100 a.k.a NOKIA YA TOCHI; ''UNAIKUMBUKA??''

Nokia 1100 maarufu kama Nokia ya tochi ndio simu iliyouza kuliko simu zote zilizowahi kuzalishwa humu ulimwenguni. Simu hii ilitengenezwa mwaka 2003 na ilibuniwa na mmarekani mwenye asili ya Bulgaria anayeitwa Miki Mehandjiysky . Kwa sasa Nokia hawaendelei kuzalisha tena modeli ya simu hii. Mpaka sasa hakuna aina nyingine ya simu iliyouza kuliko hii Nokia 1100 a.k.a Nokia ya tochi. Mpaka inaachwa kutengenezwa mwaka 2009 jumla ya simu milioni 250 zilikuwa zimeuzwa. UNAAMINI?? Hakuna aina nyingine ya simu iliyowahi kuzalishwa na Nokia au kampuni nyingine yoyote ikafikia kiwango hicho cha mauzo.Inatoka kwa mdau.

Kamamnda Kova Azungumzia Tukio La Kutekwa Dr. Ulimboka...!

Kamanda wa polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam Kamanda Suleiman Kova akizungumza na waandishi wa habari kuhusu tukio la utekaji nyara na kujeruhi lililompata kiongozi mgomo wa Madaktari Steven Ulimboka anayedaiwa kutekwa na watu watano wakati akipata kinwaji katika klabu ya Leaders Kiondoni jijini Dar es salaam. Kamanda Kova amesema Ulimboka aliokotwa na msamaria mwema ambaye hakutaka kumtaja jina lake kiusalama na kutoharibu upelelezo kuwa msamaria mwema huyo alimuokota Ulimboka katika msitu wa Mabwepande na kutoa taarifa kituo cha polisi cha Bunju, ambapo polisi aliyekuwa zamu alichukua maelezo yake na baadae Steven Ulimboka kuletwa katika hospitali ya taifa ya Muhimbili kwa matibabu zaidi. Kamanda Kova amesema jeshi la Polisi Kanda Maalum limeunda jopo maalum kwa ajili ya uchunguzi na upelelezi wa tukio hilo la utekaji nyara, kwani ni tukio la kwanza kutoke nchini, ameongeza kwamba wahusika wote watakaobainika kuhusika na tukio hilo wachukul...

UPDATE YA YALIYOMKUTA DR ULIMBOKA

UPDATE ya maelezo ya mkasa uliomkuta Dkt. Ulimboka:   Dkt. Helen Kijo-Bisimba wa LHRC akinukuliwa katika EA Redio amekariri maelezo ya Dkt. Ulimboka ambayo pia yamesikika yakitamkwa na mwenyewe (Dkt. Ulimboka Steven), kupitia kituo cha redio cha CloudsFM, kwamba walikuja watu watatu waliovalia kiraia na kujitambulisha kuwa wao ni askari. Watu hao walimchukua na kumuingiza katika gari lisilokuwa na namba na kuanza kuelekea barabara ya Bagamoyo. Huko walimfunga kitambaa usoni, kamba mikononi na miguuni kisha wakampiga huku wakimwambia amekuwa akiwasumbua kwa muda mrefu na kama wangekuwa na sindano ya sumu wangemmaliza kabisa.     --- UPDATE: Dkt. Ulimboka amefikishwa katika hospitali ya Muhimbili kwa ajili ya kupatiwa huduma. Hali yake ni mbaya ila "stable". ------ Baadhi ya watu wa shirika la Tanzania Legal Human Rights Center (LHRC) walifanya juhudi za kumtafuta kiongozi wa Jumuiya ya Madaktari Tanzania, ...

JE NI KWELI CHRIS BROWN NI MKALI KIASI KILE AU WIMBO WAKE WA ''LOOK AT ME NOW'' NDIO MKALI ?

Katika Tuzo za BET HIPHOP AWARDS zilizofanyika hivi karibuni wimbo wa ''look at me now'' wa Chris Brown ulionekana kuwa gumzo baada ya kuchukua tuzo kadhaa. Wimbo huo ulichukua tuzo ya kuwa na video kali zaidi. Na pia ulikuwa wimbo bora wa kushirikishwa( best collable). Na pia ulichukua tuzo ya kuwa  wimbo wenye 'verse' kali zaidi. Bila kusahau ulikuwa wimbo bora uliochaguliwa na watazamaji. HII YOTE INADHIBITISHA KAMA CHRIS BROWN NI MKALI? Track ya 'look at me now' inapatikana katika albamu ya Chris Brown ya ''FAME''ambayo aliitoa mwaka huu mwezi februari. Wimbo huu uliandikwa na Chris Brown mwenyewe pamoja na Buster Rhymes,Lil wayne na jamaa wengine wawili ambao ni Diplo,Jean Baptiste,Ryan pamoja na Afrojack. Ingawa Diplo na Afrojack ndio washkaji waliotengeneza wimbo huu wakishirikiana na mkali mwingine aitwaye Free School. Hii ngoma imefika mpaka kushika namba 6 katika chati maarufu na zinazoheshimika za Billbo...

New Music- Boqui ft henri soul in 'SOKUTUYOYO'

Happy Monday! A great way to kick off the monday morning with this nice, infectious song from gospel artist B.O.U.Q.U.I featuring Henri Soul titled Sokutuyoyo . Before you realize it, Sokutuyoyo sticks in your brain. Produced by Samklef Enjoy. So the music industry is getting super saturated, an unexpected turn in A country whEre musicians were once rated as hoodlums. Talents have come and gone,one hit wonders, 2 hit wonders evEn no hit wonders,Small wonder its a really congested industry. However some talents have weathered thE storm and managed to remained consistent, regardless of pressure to conform. B.O.U.Q.U.I is one of such persistent artists that are truly gifted and have stuck to their guns through thick and thin. Fresh from the world tour of 15 states in the USA 32 cities in UK and Europe And 5 states in Canada. She didn’t comE home Empty handed, she Came with yet another hit that thE talented SamKlef quickly gave life too. The song is titled SOKUTUYOYO...

Italia yafuzu kuingia nusu fainali

Timu zote mbili zilishindwa kuzitumia nafasi zilizojitokeza katika muda wa dakika 120 kufungana mabao Timu ya England ya soka imeondolewa katika mashindano ya Euro 2012, baada ya kufungwa na Italia usiku wa Jumapili katika robo fainali, kwa kufungwa magoli 4-2 ya penalti mjini Kiev, Ukraine, kufuatia muda wa kawaida na dakika 30 zaidi kumalizika kwa timu hizo mbili kutofungana. Italia sasa itapambana na Ujerumani katika mechi ya nusu fainali. Alessandro Diamanti alifunga bao la kuamua mshindi katika mikwaju hiyo ya penalti, baada ya Ashley Young na Ashley Cole kukosa kufunga mabao kupitia mikwaju waliyopiga. Vijana wa meneja Roy Hodgson ilikuwa wazi walilemewa katika mchezo mzima, lakini ni hali ya imani na uvumilivu iliwafanya kuwa na matazamio ya kuishinda...

Venus hana lake Wimbledon

Bingwa wa Wimbledon mara tano Venus Williams ameondolewa mapema baada ya raundi ya kwanza Bingwa mara tano katika mashindano ya tennis ya Wimbledon, Mmarekani Venus Williams, amesema hana nia ya kustaafu, baada ya kuondolewa katika siku ya kwanza ya mashindano ya mwaka 2012 ya Wimbledon, katika raundi ya kwanza, aliposhindwa na mchezaji kutoka Urusi, Elena Vesnina. Venus, mwenye umri wa miaka 32, na anayeugua ugonjwa unaofahamika kama Sjogren's Syndrome , alishindwa 6-1 6-3 siku ya Jumatatu. Mpinzani wake Vesnina amepangwa katika nafasi ya 79 katika orodha ya wachezaji bora zaidi wa tennis wa kike ulimwenguni. "Haiwezekani nipumzike tu na kukata tamaa," ...

Serikali Kukuza Ubia Baina ya Sekta ya Umma na Binafsi

Na Othman Khamis Ame Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inakusudia kujenga misingi imara ya kukuza ubia baina ya Sekta ya Umma na ile Binafsi ili kuwajengea uwezo Wazanzibari kushiriki kikamilifu katika shughuli za Kiuchumi Nchini. Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mh. Mohamed Aboud Mohamed ameeleza hayo wakati akiwasilisha Hotuba ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar kwa Mwaka wa fedha wa 2012/2013 katika Kikao cha Baraza la Wawakilishi kinachoendelea kwenye ukumbi wa Baraza hilo hapo Mbweni Nje kidogo ya Mji wa Zanzibar. Mh. Aboud alisema misingi hiyo { Public –Private Partnership } itakwenda sambamba na Sekta Binafsi kuwekeza kwenye Miradi mbali mbali ya Maendeleo ya Kiuchumi na Utoaji wa Huduma. Waziri Aboud alifahamisha kwamba Sekta Binafsi ni kichocheo kikubwa cha ukuaji wa Uchumi wa Taifa, hivyo kupitia uwekezaji wa Sekta hiyo Nchi itakuwa na fursa kubwa ya kuongeza...

Kwaito Ya Nape Nnauye!

Mbeya, jana.Inatoka kwa Mjengwa.

Simba Wamkatia Tamaa Yondani

WAKATI mwenyekiti wa Simba, Ismail aden Rage akijigamba kulijumuisha jina la mchezaji Kelvin Yondani katika usajili, habari ambazo Mwananchi imezipata, ni kwamba klabu hiyo imeamua kuachana na mchezaji huyo. Simba ilikuwa ikihaha kumnusuru beki huyo ambaye amekwishajichomoza Yanga na hata kuanza mazoezi wakitaka kumrejeshea fedha zake apeleke Yanga na arudi kundini. Hatua hiyo ilifikiwa baada ya Yondan kuanza mazoezi Yanga, na viongozi na wadau wakubwa wa Simba walikuwa katika hekaheka za kumrudisha kundini. Awali Habari ambazo Mwananchi ilizipata zilidai kuwa mdau mmoja wa Simba alikutana na wadau na viongozi wa Simba pamoja na Yondani mwenyewe wakimshawisi wampatie fedha, kiasi alichochukua ili azirejeshe Yanga. Chanzo cha habari kinasema kuwa wadau na wapenzi wa Simba hawakuridhishwa na hatua ya beki huyo kwenda Yanga na kwamba anahitajika kwa kiasi kikubwa Simba. Baada ya Yondani kuonyesha kuanza mapenzi mapya na Yanga, watu wa ka...

Na Gazeti la NIPASHE: Tume ya Warioba kutafuna bilioni 40/-

Na Mwandishi wetu 24th June 2012 - Kwa mwaka kila mjumbe kuvuna zaidi ya milioni 300/- – Wasio wajumbe yaani watumishi kutumia bilioni 4.3/- – Sh bilioni 2.0 kulipia nyumba wafanyakazi wa Sekretariati Serikali imefanya kufuru ya kutenga Sh. bilioni 40/- kwa ajili ya wajumbe 34 wa Tume ya Kuratibu Maoni ya Katiba. Kwa mujibu wa kasma ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba iliyoko kwenye Bajeti ya Serikali ya mwaka 2012/13. Iliyopewa jina la Vote Number 8 (Fungu namba 8), wajumbe 34 wa tume hiyo wametengewa posho ya Sh. bilioni 10 watakayolipwa kwa kipindi cha mwaka mmoja jambo ambalo baadhi ya wabunge wamesema hawaridhiki na kuhoji serikali inatafuta kitu gani kwa tume hiyo. Wajumbe wa kawaida wa tume hiyo kwa mujibu wa mchanganuo wa bajeti, watalipwa posho ya Sh. karibu 450,000 kwa siku lakini Makamu Mwenyekiti na Mwenyekiti wa Tume fungu lao ni kubwa zaidi ambalo limeongezewa viburudisho na takrima. Kwa mujibu wa taarifa za uchambu...

Liverpool to Face Tottenham Hotspur In Baltimore This July On US Tour

Liverpool and Tottenham Hotspur will play against each other in a friendly this summer in Baltimore, it was announced this morning. The two classic Premier League clubs will play on July 28, 2012 at M&T Bank Stadium in Baltimore. Kick-off time is 1pm ET. “With matches already confirmed against LA Galaxy and the New York Red Bulls, this third fixture is a great opportunity for two of the biggest names in English football to showcase the strength of the Premier League to a North American audience – something we know will appeal to our many fans that live across the USA,” said Tottenham Hotspur club chairman Daniel Levy. Read More>>

Kongamano la "jukwaa" la vyombo vya habari laanza

Kongamano linalojulikana kama Global Media Forum ambalo linawaleta pamoja wataalamu kutoka vyombo vya habari, wanasayansi na wanasiasa, limeanza leo Jumatatu (Juni 25 hadi 27 ) katika jengo la Deutsche Welle mjini Bonn " Elimu bado ni mada kuu katika suala zima la utandawazi," alitamka hayo Mkurugenzi mkuu wa Deutsche Welle, Erik Bettermann. Jinsi gani " Elimu kwa wote" lilivyo jambo muhimu, ndiyo suala kuu la majadiliano ya siku tatu miongoni mwa wataalamu kutoka vyombo vya habari, wanasayansi na wanasiasa kuanzia Jumatatu (Juni 25 hadi 27 ) katika kongamano linalojulikana kama Global Media Forum katika jengo la Deutsche Welle mjini Bonn." Habari na elimu ndiyo msingi wa harakati za chombo cha matangazo ya kigeni cha Ujerumani", anasema Mhariri mkuu wa DW, Ute Schaeffer. Kwa mujibu wa idadi rasmi ya Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa mataifa, kiasi ya watu 800 milioni hawajui kusoma na kuandika.Wakati ...

BIA YA NDOVU YAPOKEA TUZO YA DHAHABU

  Mpishi Mkuu wa Kampuni ya bia Tanzania TBL Gaudence Mkolwa, akipokea tuzo ya  kimataifa ijulikanayo kama “Grand Gold Award”kutoka kwa   Meneja wa bia ya Ndovu Special Mult Pamela Kikuli, baada ya kukabidhiwa na  Meneja wa Wateja wa kampuni ya kimataifa ya kusafirisha mizigo DHL Busegi Kulwa (kulia), jijini Dar es Salaam kushoto ni Meneja wa habari na mawasiliano Edith Mushi .   Grand Gold Award Meneja wa Wateja wa kampuni ya kimataifa ya kusafirisha mizigo DHL Busegi Kulwa, akikabidhi  tuzo ya dhahabu yenye hadhi ya juu zaidi ya ubora wa bidhaa kimataifa ijulikanayo kama “Grand Gold Award” kwa Meneja wa bia ya Ndovu Special Mult Pamela Kikuli, baada ya kinywaji hicho kinachozalishwa na kampuni ya bia Tanzania TBL, kupata tuzo hiyo kwa mara ya pili mfululizo. MENEJA  wa wateja wa kampuni ya kimataifa ya kusafirisha mizigo DHL Busegi Kulwa, amesema kampuni yao inajiskia faraja sana kufanya k...

RAIS WA SAHRAWI AWASILI NCHINI KWA ZIARA YA KIKAZI YA SIKU MBILI

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimpokea Rais wa Jamhuri ya Kiarabu ya Sahrawi Mhe, Mohamed Abdelaziz katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam jioni ya leo Jumapili Juni 25, 2012 ambapo gwaride la Kijeshi na ngoma za utamaduni zilimlaki kwa nderemo. PICHA NA IKULU

Miss Universe Tanzania 2012- The Girls

 Coming from 7 different regions of Tanzania...these are 13 of 20 contestants  All looking ultra beautiful after a thorough make-over  These girls are all amazing!! beautiful features,amazing bone structures...  Each and everyone of them with their unique beauty!  Need I say more?  Diamonds on the rough....  All girls have been STYLED by Missie Popular....Colorful pieces for chic and elegante looks  Make up done by Edna Ndibalema of Ndibs Style and the young and talented Ria.... Assisted by Irene and Edith Ndibalema The full photoshoot of all the girls will be on the Miss Universe Tanzania magazine that will be provided to all guests who will be at the event,This Friday! Do you have your ticket already?? Get one from Le Grande Casino or Call +255 767 911 123

Na Gazeti la mwananchi: Pengo: Wahuni wasiachwe kuchoma makanisa Zanzibar

ASHANGAA SMZ KUZIDIWA NGUVU, UAMSHO YAKUBALI KUSHIRIKI MCHAKATO WA KATIBA MPYA Mwadhama Polykarp Kardinal Pengo Ibrahim Yamola ASKOFU Mkuu wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo ameitaka Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), ‘kudhibiti wahuni wanaotaka kuvuruga amani visiwani humo’. Kauli hiyo ya Pengo ni ya kwanza tangu kuibuka kwa vurugu visiwani Zanzibar mapema mwezi huu, na kusababisha uharibifu wa mali, huku makanisa yakilengwa zaidi na kikundi kinachojiita cha Jumuiya Uamsho na Mihadhara ya Kiislam (JUMIKI). Pengo alitoa kauli hiyo wakati wa ibada maalumu iliyofanyika katika Kanisa la Msalabani Bagamoyo, mkoani Pwani, ikiwa ni maandalizi ya Mkutano Mkuu wa Shirika la Roho Mtakatifu, utakaofanyika kwa siku 30 kuanzia jana. Kardinali Pengo alisema, ‘wahuni hawawezi kuizidi Serikali makini’.“Makanisa yetu yamecomwa moto na watu wahuni. Kama Serikali ipo na haiwezi kuchukua hatua dhidi ya wahuni, usalama uko...

KUTOKA BARAZA LAWAWAKILISHI ZANZIBAR‏

Waziri wa Nchi na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Mwinyihaji Makame akiwa pamoja na Waziri wa Katiba na sheria wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ndani ya Baraza la Wawakilishi huko Mbweni nje ya Mji wa Zanzibar.    Mwakilishi wa Jimbo la Magomeni Salmin Awadh Salmin kushoto akibadilishana Mawazo na Mwakilishi wa Kuteuliwa Asha Bakari na (picha ya pili kulia) Katibu wa Ofisi ya Mufti wa Zanzibar Sheikh Fadhil Soraga akibadilishana mawazo na Waziri wa Biashara Viwanda na Masoko Nassor Ahmed Mazrui nje ya Ukumbi wa Baraza la Wawakilishi Mbweni nje ya Mji wa Zanzibar. Waziri wa Nchi Afisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mohd Aboud Mohd akitoa hotuba ya Makadirio na Mapato na Matumizi ya Fedha kwa Mwaka 2012/2013 huko katika Baraza la Wawakilishi Mbweni nje ya Mji wa Zanzibar. Picha na Yussuf Simai Habari maelezo Zanzibar

MADAKTARI KUANZA MGOMO…TENA!

JUMUIYA ya Madaktari imetangaza rasmi kuanza kwa mgomo usio na kikomo kuanzia kesho, huku ikidai Serikali imekataa kutekeleza madai yao yote yaliyowasilishwa katika kamati ya majadiliano iliyoundwa na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda.Wakati madaktari hao wakitangaza kurejea rasmi katika mgomo huo uliositishwa miezi mitatu iliyopita, Pinda aliliambia Bunge jana wakati akijibu Maswali ya Papo kwa Papo, kuwa mgomo huo ni batili na haukubaliki. Saa chache baada ya Pinda kutoa onyo hilo lililorushwa moja kwa moja na vituo vya televisheni na redio kutoka Dodoma, madaktari hao wakiwa jijini Dares Salaam walitangaza mgomo huo wenye lengo la kushinikiza Serikali kutekeleza madai yao. Mgomo huo ulitangazwa kwa waandishi wa habari na Dk Stephen Ulimboka, muda mfupi baada ya kukamilika kwa mkutano wa ndani wa madaktari, uliofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Jengo la Utamaduni la Watu wa Urusi. Dk Ulimboka alisema mgomo huo usio na kikomo utawahusu madaktari wa kada zote nchini,...