Kocha Arsene Wenger aliyetanganza kung’atuka Arsenal, amesema hana mpango wa kupendekeza mtu atakayerithi mikoba yake Emirates.
Akiongea kwenye mkutano wa waandishi wa habari kuelekea mchezo wa Europa League kati ya Arsenal na Atletico Madrid, Wenger pia alifichua kuwa kutangaza kwake kuondoka Arsenal hakukuja kwa utashi wake bali ni kwa msukumo wa bodi.
“Sina mpango wa kupendekeza mrithi wangu. Kwasasa sitaki kuzungumza lolote juu ya hilo,” alisema Wenger baada ya kuulizwa iwapo atapendekeza kocha mpya Arsenal.
Comments