sehemu ya Mbele ya Nyumba ya Makumbusho ya Mwalimu Julius Nyerere
Nyumba ya Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere
Watanzania wametakiwa kujiwekea mazoea kutembelea maeneo pamoja na nyumba zenye historia ili kuweza kufahamu historia ya nchini hususani Nyumba ya kumbukizi ya Mwalimu Nyerere.
Leo Arpili 6,2018 nimefika mpaka Magomeni jijini Dar es salaam sehemu iliyopo Nyumba hiyo ambapo nimezungungumza na Mhifadhi Mkuu wa Nyumba Kumbukizi ya Mwalimu Nyerere,Neema Mbwana ambapo amesema nyumba hiyo imesheheni historia mbalimbali zitakazosaidia watu kufanya utalii.
Aidha Mhifadhi Neema amesema wanakumbana na changamoto kutokana na watanzania kutokuwa na muamko wa kwenda kufanya utalii kwenye nyumba hiyo ili kuweza kujifunza pamoja na kuyatizama matukio mbalimbali ya kihistoria aliyoyafanya Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere.
Amewataka watanzania kufika kwenye nyumba hiyo kwani wataweza kufahamu historia kamili ya nchi yao ikiwemo kujionea baadhi ya vitu ambavyo alikuwa kivitumia wakati wa uhai wake.
Nyumba ya Mwalimu Nyerere ilijengwa mwaka 1959 ambapo ilikuwaKingine ambacho kinaifanya nyumba hii kuwa ya kihistoria ni pamoja na kuwa alijinyima wakati akijenga, aliishi kwa muda wa miezi minane tu kabla ya kuteuliwa kuwa Waziri Mkuu wa Tanganyika Januari 1, 1960.
Comments