Vyama vya siasa vya MLC, UNC, CNB, UDPS vilitoa tamko la pamoja siku ya Jumatano, Aprili 11, 2018 kukataa mfumo wa kupiga kura kwa kugusa kwenye skrini ya mashine. Kwa upande wa vyama hivi vya upinzani vimesema “teknolojia hii ni hatari kwa udanganifu na wizi wa kura wa haraka”.
Hivi karibuni Korea Kusini ilionya dhidi ya matumizi ya “mashine za kupigia kura” zinazotarajiwa kutumiwa wakati wa uchaguzi unaopangwa kufanyika nchini DRC mwishoni mwa mwaka huu.
Mashine hizo zimetengenezwa na kampuni moja huko Korea Kusini, huku ikisema kuwa inaogopa kuwepo matokeo mabaya ya uchaguzi wa Desemba 23 ambao ndio utatatamtisha utawala wa Rais Joseph Kabila.
Kauli Hiyo ilitolewa wakati kukiwa na tetesi kuwa kuna uwezekano wa kufanyika udanganyifu ama wizi wa kura nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kwa faida ya vyama vinavyomuunga mkono rais Joseph kabila Kabange.
Seoul inaamini kuwa matumizi ya mashine hizi inaweza kusababisha machafuko zaidi nchini humo na kufanya kutoa matokeo yasiyo ya kweli, Taarifa kutoka ubalozi wa Korea Kusini nchini DRC huko Kinshasa imesema
.- Get link
- X
- Other Apps
- Get link
- X
- Other Apps
Comments