KIUNGO wa Simba Mnyarwanda Haruna Niyonzima 'Fabregas' huenda akaukosa mchezo wao wa Aprili 29 dhidi ya watani wao Yanga kutokana na kufiwa na dada yake anayeitwa Sumaye kwao Rwanda.
Niyonzima ambaye leo mchana imembidi asafiri kurudi Dar es Salaam akitokea Morogoro ambako kikosi chao cha Simba kimeweka kambi kwa ajili ya mchezo huo na alitarajia kuondoka mchana.
"Nimepata matatizo bwana, nimefiwa na dada yangu nyumbani Rwanda na hivi sasa niko hapa nyumbani nikijiandaa kwa ajili ya safari. Kwa sababu ni jambo la kushtukiza ndiyo nahangaikia ndege kuona kama naweza kuondoka,"anasema Niyonzima aliyesajiliwa msimu huu akitokea Yanga.
Simba na Yanga zinacheza wikiendi hii ambapo kama Niyonzima ataondoka kuna uwezekano mkubwa wa kuukosa mchezo huo ambao kwa kawaida huwa na ushindani mkubwa.
Comments