Arsenal imeilamba Southampton 3-2 katika mchezo wa funga nikufunge wa Ligi Kuu ya England uliochezwa Emirates Stadium.
Southampton ilikuwa ya kwanza kupata bao la kuongoza dakika ya 17 kupitia kwa Shane Long, lakini Pierre-Emerick Aubameyang akaisawazishia Arsenal dakika ya 28 huku Danny Welbeck akidumbukiza wavuni bao la pili dakika kumi baadae.
Charlie Austin akaisawazishia Southampton dakika ya 73, lakini Arsenal ikahitimisha ushindi wao dakika ya 81 kupitia kwa Welbeck.
Comments