Na Francis Peter
JESHI la Polisi nchini limesema watu 9 wamefariki kutokana na mvua
zinazoendelea kunyesha katika maeneo mbali mbali ya jiji la Dar es
Salaam.
Kamandawa kanda maalum ya Dar es salaam Lazaro Mambosasa
Hayo yamesemwa jijini hapa jana na kamanda wa Polisi kanda maaalum ya
Hayo yamesemwa jijini hapa jana na kamanda wa Polisi kanda maaalum ya
Dar es Salaam SACP Lazaro Mambosasa alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari
ambapo alisema Aprili 14 majira ya 21:45 huko maeneo ya Segerea mataa wa
mjimwema watu wawili ambao ni Grace au mama Elias (30) na Abdulrazak Ally
(4) wamefariki baada ya kuangukiwa na uzio wa ukuta wakati wamelala ndani ya
nyumba.
Alisema ukuta huo wa uzio wa nyumba uliangukia nyumba ya ya vyumba vitano inayokaliwa
na wapangaji ambapo katika tukio hilo watu wanne walijeruhiwa na kupelekwa
hospitali ya amana kwa matibabu.
"Miili ya marehemu ilipelekwa hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa hifadhi na pia
mnamo Aprili 2018 majira ya saa 22:20 huko maeneo ya Gga Salasala nyumba ya chumba
kimoja ilianguka na kusababisha kifo cha mtu mmoja aitwaye Mikidadi Hija(44),"alisema
SACP Mambosasa.
SACP Mambosasa alisema katika tukio lingine mnamo Aprili mwaka huu majira ya saa 13:00
huko maeneo ya kigogo Mwanaidi Seif (24) aliangukiwa na ukuta wa nyumba akiwa ndani
na kusambabisha kifo.
Aidha Jeshi la Polisi limesema kuwa mnamo Aprili 15 mwaka huu majira ya saa 16:00 huko
maeneo ya Temeke Sadick Ally (36)aliteleza na kutumbukia katika daraja la mto Kizinga
lililokuwa limejaa maji na kusababisha kifo ambapo jitihada za kuutafuta mwili wa marehemu
bado zinaendelea.
Pia SACP Mambosasa aliendelea kupambanua katika taarifa hiyake kuwa mnamo Aaprili
16 mwaka huu majira ya saa 05:45 maeno ya Mbagala misheni mtu mmoja Nasri Ally Haji 9
mwanafunzi wa shule ya msingi Bbokorani alifariki baada ya kuangukiwa na ukuta wa
nyumba akiwa amelala.
Vile vile kamanda huyo wa Polisi Kanda maalum Dar es Salaam alisema kuwa mnamo
Aprili 15 majira ya saa 11:00 mwaka huu huko Kinyerezi kwenye bonge la mto
Kinyerezi mtu mmoja wenye jinsia ya kiume ambaye jina lake halikufahamika,
anaye kadiriwa kuwa na umri wa miaka 25 hadi 35 alikutwa amekufa kutokana na
kusombwa na maji.
Taarifa hiyo ya mvua zinazoendele kunyesha jijini Dar es Salaam zimeeleza kuwa
mtu mmoja jinsia ya kiume ambaye jina lake halikufahamika anayekadiriwa kuwa
na umri kati ya miaka 25 hadi 35 alikutwa amekufa huko Kawe Mezi Beach A, baada ya
kusombwa na maji ambapo mwili huo umehifadhiwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.
Hli hiyo ya mwendelezo wa mvua imetaja kuwa Aprili 16 mwaka huu huko Kawe Salasala
Amina Said (28) amefariki baada ya kuangukiwa na ukuta wa nyumba akiwa amelala nyumbani
kwake.
wakati huo huo taarifa ya Kikosi Cha Usalama Bara Barani Kanda Maalum ya
ukamataji wa makosa ya barabarani kuanzia Machi 30 mwaka huu hadi Aprili 12 mwaka
huu kimetaja idadi ya magari yaliyokamatwa kuwa ni 32,361 ambapo idadi ya Pikipiki
zilizo kamatwa ni 906 huku Dala Dala zikiwa ni 12,321 magari mengine binafsi na Malori
ni 20,040.
Bodaboda zilizofikishwa mahakamani kwa makosa ya kutovaa helment na kupakia mshikaki
zimetajwa kuwa ni 60 na kuwa jumla ya makosa yaliyokamatwa ni 35,115 ambapo
fedha na tozo zilizopatikana ni 1,053,450,000/=.
Comments