Polisi mjini Toronto nchini Kanada wamethibitisha kuwa watu 10 wameuwawa baada ya dereva wa gari kuwagonga kwa kudhamiria. Katika tukio hilo Watu wengine 15 wameripotiwa kujeruhiwa, ambapo taarifa kutoka hospitali ya Sunnybrook iliyopo katika mji huo zimefahamisha kwamba baadhi ya majeruhi wapo katika hali mbaya.
Dereva wa gari hilo alijaribu kukimbia lakini polisi walifanikiwa kumkamata. Kaimu mkuu wa polisi wa Toronto Peter Yuen amesema dereva huyo anachunguzwa na ametoa mwito kwa walioshuhudia tukio hilo kujitokeza na kutoa taarifa zaidi
.
Comments