siku ya taalum.
Ili kuendelea kukuza ukuzaji wa sekta ya utalii na ajira nchini,Chuo
cha Taifa cha Utalii kimeandaa tamasha la siku ya taaluma lenye ujumbe
wa fursa za Ajira kwa vijana kupitia taaluma ya Ukarimu na utalii.
Hayo yameelezwa leo na Kaimu Mkurugenzi wa Mafunzo na shughuli za
kitaalam katika chuo hicho,Stephen Madenge wakati akikzungumza na
waandishi wa habari jijini Dar es salaam,ambapo amesema lengo ni
kuhakikisha wanawaleta wadau mbalimbali karibu kupitia sekta ya utalii.
Magenge amesema sekta ya utalii nchini haijapungua kwani imeendelea kufanya
vizuri kwa kuweza kujipatia watalii ukilinganisha na nchi zinazozunguka
Afrika Mashariki hivyo wataendelea kutoa elimu ya utalii kwa watanzania.
"Kwa kutumia tamasha hili wanafunzi wataonesha kwa vitendo uhodari wa taaluma
zitolewazo chuoni ikiwa ni pamoja na Live Cooking,Cocktail na pastry product
makini,wine testing and testing preparatioin lakini pamoja na hayo kutakuwa
na uwasilishwaji wa mada za ukarimu na utalii kutoka kwa wataalamu mahiri wa
sekta ya ukarimu na utalii wa hapa nchini"amesem Mkurugenzi Madenge
Amesema kupitia tamasha hilo wanategemea kuwaunganisha na kuwaleta kwa
pamoja wadau mbalimbali wa chuo kama hotel,kampuni za kitalii,banki,kampuni
za mawasiliano,taasisi,idara na wizara mbalimbali wanafunzi wa shule za
sekondari,wazazi na jamii kwa ujumla.
Kwa upande wake Mratibu wa tamasha hilo la siku ya Taaluma Eunice Ulomi
amesema wataendelea kuwafundisha wanafunzi elimu ya utalii ikiwemo ya
utamaduni ili kuweza kutangaza asili ya mtanzania jambo litakalosaidia
kuwavutia watalii.
Martina Hagweti ni Mkuu wa kampasi ya Temeke jijini hapa amesema
wanawahamasisha watanzania kuwa na dhana ya kujiewekea mazoea ya
kutembelea vivutio vya utalii vilivyopo nchini ili kuifahamu nchi yao.
Chuo cha Taifa cha Utalii (NCT) ni wakala uliopo chini ya Wizara ya
Maliasili na Utalii wenye dhamana ya kutoa mafunzo ya ukarimu na utalii
nchini lakini pia kinatoa ushauri wa kufanya tafiti katika fani ya ukarimu
na utalii na hivyo tamasha ya siku ya taaluma linatarajiwa kufanyika tar
27/4 mwaka huu ambapo mgeni anatarajiwa kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili
na Utalii Generali Gaudence Milanzi.
Baadhi ya masomo ya kuendelea kukuza ukuzaji wa sekta ya utalii
na ajira nchini yanayotajwa kutolewa na chuo hicho ni .
CERTIFICATE COURSE IN HOTEL MANAGEMENT (miezi 9)ambapo kozi zakeni
1.1. Accomodation Operation.1.2 Front Office Operation,1.3. Food and Beverage
Services,1.4 Introduction to Tourism kwa ada nafuu ya Tsh. 800,000/=
Mambo mengine katika masomo ni pamja na 2.0 HOUSE KEEPING MANAGEMENT
(mwezi mmoja ). kwa ya Tsh 100,000/=,3.0 CERTIFICATE COURSE IN
TOURISM MANAGEMENT (miezi 9).
Kozi zingine zimetajwa kuwa ni Introduction to Tourism 3.1, Travel and Air
Ticketing 3.2, Tour Planning 3.3.pamoja na Customer care 3.4,Communication
skills 3.5 kwa ada ya Tsh.700,000/=.
Comments