Wakati dunia nzima ikiamini kuwa jina la mtoto ni haki ya wazazi au ndugu wa karibu wa baba au mama kuchagua jina walipendalo, Hii ni tofauti kabisa na wanandoa wawili mjini Toulouse nchini Ufaransa ambao wamejikuta wakifikishwa kwa pilato kwa kumbatiza mtoto wao wa kiume jina la ‘JIHAD’ na kuamriwa kufuta jina hilo kwenye cheti cha kuzaliwa cha mtoto wao na kumbatiza upya.
Uamuzi huo uliofanywa na Mahakama mjini Toulouse umekuja baada ya askari polisi mjini humo kubaini jina la mtoto huyo la ‘JIHAD’ ni jina litakaloharibu maisha ya mtoto huyo baadaye na usalama wa taifa. Na kuamua kuwapeleka wazazi hao mahakamani kujibu mashtaka baada ya kufanya nao mahojiano kwa miezi kadhaa.
Wazazi hao walifikishwa mahakamani mjini Toulouse wiki iliyopita kwa kumbatiza mtoto majina ambayo yamekatazwa kutumika nchini humo na polisi kwa sababu za kiusalama. Mfano wa majina hayo ni Nutella, Fraise na mengine unaweza kusoma zaidi HAPA .
Mahakama hiyo imewaamuru wazazi hao kufuta jina hilo kwenye cheti cha kuzaliwa cha mtoto huyo na kumbatiza ‘JAHID’ badala ya jina la ‘JIHAD’ kama wangependa kufanya hivyo.
Kwa mujibu wa mtandao wa Local.fr tayari wazazi hao jana Aprili 16, 2018 walikubaliana na ombi la Mahakama kubadilisha jina hilo na tayari mtoto kasajiliwa kwa jina Jahid.
Hii sio kesi ya kwanza nchini Ufaransa kwa wazazi kukamatwa na polisi kisha kufikishwa mahakamani kwa kuwabatiza watoto wao majina ya kichochezi au yenye kushabihiana na uvunjifu wa amani, ambapo mwaka 2013 mzazi mmoja mjini Roubaix aliyembatiza mtoto wake jina la JIHAD na kisha kumvalisha fulana yenye maandishi yaliyosomeka ‘Je suis une bombe’ yaani ‘Mimi ni bomu’, kufungwa jela mwezi mmoja na kulipa faini ya dola $2,000 kwa kuchochea uhalifu.
Comments