WAZIRI wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe Dr Harrison Mwakyembe, ameyataka makampuni mbali mbali kujitokeza katika kudhamini
Shindano maarufu la Miss Tanzania 2018 .
Hayo yalisemwa na Dr Mwakyembe juzi usiku Katika uzinduzi wa shindano hilo katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa Dar es Salaam,alisema anashukuru uongozi wa Kampuni ya The Look Company Limited kwa kumwalika kuwa mgeni rasmi katika usiku huo mwaka huu .
Alisema amefurahi kusikia kwamba waandaaji wa awali wa Miss Tanzania kupitia kampuni ya LINO International Agency wameachia ngazi na kupisha The Look Company Limited inayoongozwa na Bi Basila Mwanukuzi ambaye ni mwanadada aliyenyakua taji la urembo la Miss
Tanzania mwaka 1998.
"Naomba sasa nichukue fursa hii kuyaomba tena Makampuni mbali mbali kujitokeza kwa wingi kudhamini
mashindano haya , kama vile mabenki,kampuni za mawasiliano ya simu ,hoteli pamoja Wabunifu mali mbali
wa mavazi,"alisema Dr Mwakyembe.
Dr Mwakyembe alisema kuwa mbali na kuomba makampuni mbali mbali kujitokeza ataongea na uongozi wa Shirika la ndege la Air Tanzania kutoangaika kutafuta warembo wa kuhudumia ndege zetu nchini wakati tunao waliopitia chujio gumu la Miss Tanzania.
Aidha alisema Mrembo wa Taifa atakayeshinda shindano hilo, mwakahuu, mbalina kujihakikishia ajira
Air Tanzania,atawakilisha nchi katika mashindano ya dunia ya urembo na hivyo kulitangaza jina la nchi.
"Basilanakutakia mafanikio makubwa na wathibitishie wote kuiletea sifa na heshima nchi yetu, wanaodhani timu mpya ya Miis Tanzania ni nguvu ya soda nyie ni hapa kazi tu,"alisema Dr Mwakyembe.
Aliongeza kuwasema kuwa alielezwa kuwa miaka yanyuma Wizara yaUtalii Kupitia Bodi ya Utalii Tanzania,
Shirika la TANAPA,iliwahi kudhamini mashindano hayo kwa miaka miwili mfululizo mwaka 2009 na 2010 .
Ambapo alisema sasa ameviomba tena vyombo hivyo pamoja na Kituo cha Uwekezaji Tanzania (ITC) kujitokeza kuhamasisha mashindano hayo na hivyo kujitangaza Tanzania kwa utalii na uwekezaji nchini.
Waziri huyo wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo alieleza kuwa amesikia kutoka kwa Mkurugenzi wa TheLook kuwa mashindano hayo yanahitaji sana kuungwa mkono na serikali , makampuni mbali mbali na wadhamini wa kutosha ili kuyafanya yawe na kiwango cha Kimataifa na upande wa serikali tayari hakuna tatizo inawahakikishia ushirikiano wa karibu kupitia BASATA.
Dkt. Mwakyembe ameshukuru pia mchango wa muda mrefu wa makampuni makubwa kama :"White sands Hotel, Kampuni ya Sigara Tanzania (TCC);Kampuni ya Bia Tanzania (TBL),Ocean Sandals,Vodacom Tanzania.
Pia aliyataja makampuni mengine kama Tanzanite one,D.T.DOBBIE,Paradise Hotel,Giraffe Hotel nakuwa
kwa sasa ni wakati mwinginewa kuendelea kujitokeza tena kudhamini.
Comments