Barcelona imeichapa Valencia 2-1 na kuweka rekodi mpya La Liga ya kucheza mechi 39 bila kufungwa.
Sifa juzi zimwendee Philippe Coutinho ambaye alikuwa mpishi wa magoli yote mawili yaliyofungwa na Luis Suarez dakika ya 15 na Samuel Umtiti kunako dakika ya 51.
Dani Parejo akaifungia Valencia bao la kufutia machozi ukingoni mwa mchezo kupitia mkwaju wa penalti.
Comments