Jumla ya wanafunzi 50 wa Chuo cha Taifa cha Utalii leo wawepewa vyeti vya kuhitimu mafunzo ya udereva pamoja na mafunzo ya upishi katika mahali yaliyofanyika jijini Dar es salaam.
Wanafunzi hao ambao wamehitimu hii leo mafunzo hayo,kati yao wanafunzi 25 wamejifunza mafunzo ya udereva huku 25 wengine wakijifunza mafunzo ya upishi.
Akizungumza Mgeni rasmi wa hafla hiyo Mkurugenzi wa Jiji la Dar es salaam Bi.Sipora Liana amesema wanafunzi hao ni vyema wakashirikiana na jiji ili kuweza kufanya kazi kwa pamoja katika kuendeleza sekta ya utalii.
Bi Sipora amesema mafunzo hayo ambayo wameyapata kwenye chuo hicho yatawasaidia katika shughuli mbalimbali za utalii lakini pia amewataka kujiendeleza kilugha ili kuweza kuendelea kutoa huduma bora.
Awali akizungumza Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Chuo Cha Taifa Cha Utalii DK.Shogo Mlozi Sedoyeka amesema wataendelea kutoa mafunzo ya utalii kwa wanafunzi ikiwemo mafunzo ya ukarimu ili kuendelea kukuza sekta ya utalii nchini.
Kwa upande wao baadhi ya wahitimu wa mafunzo hayo wamekishukuru chuo Cha Taifa cha Utalii pamoja na Halmashauri ya jiji kwa kuweza kuwa na ushirikiano katika kuwapatia mafunzo.
Hata hivyo wanafunzi hao ambao wamepatiwa cheti hii leo wametakiwa kuendelea kuwa wazalendo kwa nchi yao katika kutangaza utalii huku akisema ni vyema wakawa walinzi wa utalii ili kuiletea nchi heshima.
Comments