Amber Rudd Waziri wa mambo ya ndani wa Uingereza ametangaza
kijiuzulu hapo jana Jumapili kufuatia kashifa dhidi ya maafisa wa nchi
hiyo kuwahusisha kimakosa wahamiaji kutoka nchi za Carribean na sehemu
ya mchakato wa kuwaondoa wahamiaji wanaoishi nchini humo kinyume cha
sheria.
Waziri Mkuu Theresa May amekubali kujiuzulu kwa Amber Rudd ambaye
amekuwa akishinikizwa na chama cha Labor kujiuzulu alikuwa akitarajia
kutoa maelezo bungeni leo Jumatatu kuhusiana na kashifa hiyo iliyogonga
vichwa vya habari nchini Uingereza kwa siku kadhaa. Kashifa hiyo
inafuatia gazeti la Guardian kuripoti kuwa baadhi ya watu waliohamia
Uingereza wakitokea nchi za Carribean miongo kadhaa iliyopita baada ya
vita kuu vya pili vya dunia wanatishiwa kufukuzwa kutokana na
kutowasilisha nyaraka zinazothibitisha kuwa wana haki ya kuendelea
kusalia nchini humo.
Comments