Diamond Platnum aliyevalia suti nyeusi akimpa mkono Alikiba aliyevalia kanzu nyeupe
Aprili 22, 2018 kwenye viwanja vya Leaders jijini Dar es salaam wasanii na wadau mbalimbali nchini wamejumuika kwa pamoja kuuagaa mwili wa Muigizaji wa filamu na Video Vixen, Agness Gerald Masogange ambaye amefariki dunia siku ya juzi.
Licha ya wasanii wengi kujitokeza kumeibuka kelele kwenye msiba huo mara baada ya mahasimu wawili wa muziki wa Bongo flavor Tanzania Alikiba pamoja Diamond Plutnumz mara baada ya kupeana mikono.
Katika msiba huo Msanii Alikiba amezungumza mengi ikiwemo na kuwashauri wasanii wenzake katika suala zimala kufikiria kuwa kifo kipo hivyo ni vyema kila msanii akafanya maandalizi sahihi
“Nachopenda kuwaambia kila mmoja wenu tufanye yote ambayo tunaona ni muhimu hapa duniani lakini tumkumbuke Mwenyezimungu lazima akumbukwe kila wakati”Amesema Alikiba wakati akitoa hotuba yake kwenye msiba
Kwa upande wake Msanii Diamond Platnumz amesema Marehemu Masogange licha ya watu kumpenda sana ila Mwenyezimungu kampenda zaidi.
“Kwa sisi waislamu tunasema kifo ni ibada hivyo tupo duniani tunapita tusijidanganye sababu tunaimba muziki hivyo ni vyema tutengeneze mazingira mazuri hapa duniani”amesema msanii Diamond
Comments