Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Charles Mwijage amezindua mpango mkakati wa Baraza la nafaka la nchi za ukanda wa Afrika Mashariki(EAGC
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Bw. Charles Mwijage
jana amezindua mpango mkakati wa Baraza la nafaka la nchi za
ukanda wa Afrika Mashariki(EAGC)Uku lengo la mkutano ukiwa ni
kuimarisha uhusiano wa kibiashara,kuongeza kiasi cha mauzo
yatakayoweza kuuzwa nchi za ng'ambo na kuboreshwa mazingira
mazuri ya biashara kati ya nchi hizo zenye ujumla wa takribani 10.
Hayo yalisemwa Dar es Salaam jana na Bw. Charles Mwijage wakati wa
Mkutano huo wadau wa nchi hizo uliowalenga wakulima,wazalishaji pamoja na
wasindikaji katika ukanda huo.
Alisema zao la Mbaazi limekuwa na soko kubwa katika nchini za Uarabuni
na Ulaya ambapo juhudi kubwa zimenza kuelekezwa huko pamoja na soko
lingine lenye wakazi wengi wenye asili ya Kihindi.
"Kwa sasa mpango mkakati ni kujihakikishia kuwa na soko kubwa zaidi
katika nchi za ng'ambo ambapo huu ni mkakati wa kunzia 2018 hadi kufikia
2022,"alisema Waziri Mwijage.
Mwijage alisema kuwa mpango wa EAGC kwa sasa utakuwa wenyetija
kubwa kutokana na mipango yake kuendelea kukua katika utaratibu
wa mkakati huo.
Kuhusu nchini Tanzania alisema kuwa mipango inaendelea vyema
katika taratibu za ukuaji wa kilimo ambapo ameitaja Aprili 30
mwaka huu Waziri Mkuu. Majaliwa Kassim Majaliwa atazindua ujenzi
wa magala ya chakula Mkoani Dodoma.
Ambapo Waziri huyo ameeleza kuwa ukikamilika utakuwa umeweza
kusababisha kuondoa woga wa nchi yetu kwa wakulima kuuza
nafaka zao nje ya mipaka tofauti na hali ya wakulima kwa soko
la mipakani kwa sasa.
"Kuwa na bajeti ndogo katika suala la kilimo napo kunaweza kuwa
chanzo cha kutopeleka mbele juhudi za kufikia malengo makubwa
ya kilimo ,"alisema Waziri Mwijage.
Alisema ujenzi wa magala katika maeneo maeneo mbali mbali kwa
sasa ni mipango ya serikali kujenga magala hayo kwani yatasaidia
sana kujua wingi wa chakula nchini kwani katika Afrika Mashariki
katika miezi tisa kila mwaka,lazima huwa linatokea eneo fulani kupata
njaa.
Nye Mkurugenzi Mtendaji wa Baraza la nafaka la nchi za ukanda wa Afrika
Mashariki(EAGC),Gerald Masila alisema taasisi hiyo imekaa kwa zaidi
ya miaka 9 hadi sasa kwa hiyo hatua za kufikia malengo makubwa ni
za mihimu wanataka kuwa na nafasi kubwa ng'ambo.
"Tanzania Kenya huwa ni wanunuzi wakubwa wa zao la nafaka EAGC
wamekuwa wakimpambania mkulima pia kuuza mazao yake,"alisema Masila.
Comments