WAZIRI wa Maliasili na Utalii Dk.Hamisi Kigwangala jana alishiriki
katika mkutano wa kamati ya maandalizi ya tamasha la mabara litakalo
fanyika nchini Ufaransa Julai mwaka huu.
Hayo yalisema na wazili Kigwangala katika mkutano huo uliofanyika
Jjini Dar es Salaam jana ambapo alisema kuwa tanzania itakuwa ni
moja wapo katika ushiriki wa tamasha hilo ambapo jumla ya nchi 54
zitashiriki kuonesha urithi wake.
WAZIRI wa Maliasili na Utalii Dk.Hamisi Kigwangala
Alisema tamasha hilo litakuwa na utamaduni wa urithi wa asili na
kuwa kamati hiyo imehusisha nchi 7 zikiwemo Kenya ,Tanzania ,Ivery
Coast.
Hivi karibuni Kigwangala alisema kuwa sekta ya utalii imekuwa
mhimili muhimu katika ukuaji wa uchumi wa Tanzania ambapo kwa
mwaka 2017 sekta ya utalii imechangia dola za kimarekani Bilioni
2.1 takriban asilimia 25 ya fedha za kigeni .
"Kupitia tamasha hilo la Mabara Urithi wa Taifa la Tanzania tutaweza
kuutangaza vema mambo kama urithi wa lugha , ngoma zetu za asili
tutaweza kuvitangaza vema,"alisema Kigwangala.
Kigwangala alisema kuwa kuelekea mwezi septemba
tayari amezindua kamati ya kitaifa ya kuandaa Mwezi
maalumu wa maadhimisho ya Urithi wa Taifa la Tanzania
ambapo kuppitia tamasha la mabala wataweza kujifunza
mambo zaidi.
Pia miji ya kihistoria kama vile Bagamoyo na Kilwa,
michoro ya miambani, Kondoa na mapango ya Amboni.
Aliongeza Tanzania ikiwa na zaidi ya makabila 120 imejaliwa kuwa
na anuaia za mila, desturi, vyakula, misemo, imani, mavazi,
nyimbo, ngoma za aina mbali mbali na matumizi ya lugha ya
Kiswahili katika kuunganisha Watazania.
Comments