Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ametengua uteuzi wa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa Mohamed Maje kwa kilichoelezwa kushindwa kutimiza majukumu yake.
Taarifa ya kutenguliwa kwa uteuzi wa Maje imetolewa na Katibu Mkuu wa Tawala za mikoa na serikali za mitaa TAMISEMI Mussa Iyombe, ambapo amesema Maje ameisababishia hasara serikali ikiwamo kushindwa hata kukusanya mapato ya serikali.
“Hata makusanyo ya mwaka huu hatuijui anapeleka wapi hadi leo amekusanya asilimia 24 tu katika halmashari ya Kongwa na Mpwapwa licha ya kuwa na vyazo vingi vya mapato.”
Iyombe ameongeza kwa kusema Mkurugebnzi huyo kwa sasa yupo chini ya uchunguzi.
Comments