Rais wa Tanzania Dkt John Magufuli ameupuuzilia mbali waraka wa maaskofu uliotolewa wakati wa kuanza kwa msimu wa Pasaka
Rais wa Tanzania Dkt John Magufuli ameupuuzilia mbali waraka wa maaskofu uliotolewa wakati wa kuanza kwa msimu wa Pasaka akisema hauna msingi wowote ule.
Aliendelea kwa kusema pia kwamba mbona hakuna aliyetoa waraka wakati mauwaji ya Kibiti yakiendelea.
Rais Magufuli amesema hayo katika hafla ya kuweka jiwe la msingi wa ujenzi wa rada za kiraia uliofanyika jijini Dar es Salaam.
Majibu yake kwa waraka wa maaskofu aliyatoa wakati akiwapongeza wasaidizi wake, mawaziri, viongozi wa ulinzi na usalama pamoja na wasaidizi wengine, ambao amewasifu kwa kuendelea kutimiza majukumu yao.
"Wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama ndio maana tuko salama leo, ilifikia mahali hata kwenda Kibiti tu ni kazi. Hatukuona mtu yeyote analaani," amesema Dkt Magufuli.Source BBC
Comments