Mohamed Salah Mchezaji wa Klabu ya Liverpool ameshinda tuzo ya mchezaji bora wa kiume wa mwaka inayotolewa na Shirikisho la wachezji wa kulipwa nchini Uingereza, Proffessional Footballers Association (PFA). Hii ni tuzo nyingine tena baada ya kushinda Tuzo ya mchezaji bora wa Afrika anaechezea ligi ya nje ya Afrika iliyotolewa na BBC, lakini pia ni baada ya kuibuka mchezaji bora wa EPL kwa mwezi March.
Katika tuzo hiyo, Salah anaweka rekodi ya kuwa mchezaji wa kwanza raia wa Misri na mchezaji wa 7 wa Liverpool kushinda tuzo hiyo, ambapo tuzo hiyo imekuwa ikiwaniwa na wechezaji wengi na wakubwa katika soka duniani akiwemo, Harry Kane wa Tottenham Hotspur, David De Gea, Golikipa wa Manchester United, Kevin De Bryune, David Silva na Leroy Sane viungo washumbuliaji wa mabingwa wa Ligi kuu England Manchester City.
Naye Leroy Sane amejishindia tuzo ya mchezaji bora chipukizi wa soka nchini Uingereza na kuwashinda Sterling wa Man City na Marcus Rashford wa Manchester United
.
Comments