Naibu waziri wa afya, jinsia wazee na watoto Dkt, Faustin
Ndugulile ameitaka jamii kuonyeshwa upendo na mapenzi mema watoto walio na
ugonjwa wa usonji kwani no wana haki ya kupatiwa malezi bora kama watoto
wengine.
Ameyasema hayo wakati akizungumza na kituo kimoja cha
redio Mkoani Dodoma ambapo amedai kuwa ugonjwa huo unawapata watoto
wadogo na ni ugonjwa unaohitaji watoto kuonyeshwa upendo pamoja na kuwajengea
uwezo ili waweze kuwa raia wazuri wa baadae.
Akizungumzia ugonjwa huo DKT Ndugulile amesema ugonjwa huo hauna
tiba huku akidai kuwa dalili za ugonjwa huo hubainika pale mtoto anapokuwa na
mwaka mmoja au zaidi na moja ya dalili hizo ni pamoja na kushindwa kuongea.
Hata hivyo Ndugulile amesema serikali inatambua uwepo wa
ugonjwa huo na tayari hatua zimeanza kuchukuliwa ikiwa ni pamoja na kutoa elimu
kwa walimu ili kuyafahamu makundi ya watoto hao hali itakayosaidia kuyatambua
mahitaji maalum yanayopaswa kutolewa kwa watoto hao.
Sanjari na hayo amesema serikali inaendelea kuhamasisha jamii
kuutambua na kuuelewa zaidi ugonjwa wa usonji pamoja na kuchukua hatua kwa watu
wenye mahitaji maalumu kwenye jamii za kuhakikisha wanapata mahitaji muhimu
kama elimu na afya
Aidha Dkt Ndugulile ameyasema hayo mapema leo ikiwa ni siku
chache tu zimepita tangu kuadhimishwa kwa siku ya ugonjwa wa usonji nchini
ambapo maadhimisho hayo hufanyika kila mwaka ifikapo april 2.
Comments