Mkuu wa Wilaya ya Ilala jijini Dar es salaam Sophia Mjema(Aliyekaa kwenye picha akiandika)
Baadhi ya viongozi mbalimbali wa Halmashauri waliokuwepo kwenye uzinduzi huo aliyekaa wa pili kushoto kavalia tisheti nyeupe ni Afisa Habari na Mahusiano Manispaa ya Ilala Tabu Shaibu
wafanyabiashara waliohudhuria kwenye uzinduzi huo
ramani ya soko hilo la kisutu linalotarajiwa kujengwa
Na Mussa.N.Khalid
Mkuu wa Wilaya ya Ilala jijini Dar es salaam Sophia Mjema leo amefanya uzinduzi wa ujenzi wa soko la Kisutu litakalokuwa na gorofa nne pamoja na kuwa na uwezo wa kuchukua wafanyabiashara zaid ya 1,500.
Mkuu wa Wilaya Mjema amefanya uzinduzi huo na kuzungumza na wafanyabiashara mbalimbali ambapo amewataka kuonyesha ushirikiano ikiwemo kuweza kupisha ujenzi wa soko hilo kwani mpaka sasa mkandarasi ameshapatikana na anatarajiwa kuanza kazi tar 15/4 mwaka huu.
Aidha DC Mjema amesema lengo la serikali ni kuziwezesha halmashauri kuweza kujitegemea zenyewe katika mapato yake ya ndani katika kujiendesha yenyewe ambapo ameeleza kuwa wameazimia kujenga masoko matatu makubwa likiwemo hilo la Kisutu.
Amewaambia wafanyabiashara wa kisutu kuwa soko lao litakuwa bora na la kisasa hivyo waendeleea kufanya kazi kwa bidii kwani fursa ndio hiyo wameipata.
Soko la Kisutu lilianzishwa mwaka 1964 likiwa na idadi ndogo ya wafanyabishara,kwa sasa soko hilo linajumla ya wafanyabishara 633 wa nje na ndani ambapo inajumuisha wafanyabiashara 201 ni wa kuku hai na kuchinja na wafanyabiashara wengine za nafaka,mbogamboga na matunda jumla yao ni 432.
Comments