MFARANSA wa Simba, Pierre Lechantre buana, kumbe hataki utani kabisa,
kwani jana asubuhi wakati kikosi chake kikianza safari kuelekea Njombe
kuwafuata Njombe Mji aliamua kufanya jambo moja ambalo mashabiki wa
Simba huenda wasiamini.
Kocha huyo mapema asubuhi kabla ya safari hiyo watakayofikia kwanza
Iringa kabla ya kuutafuta mji wa Njombe, alitangaza majina ya wachezaji
22 na kuwapiga chini wengine wanne waliokuwa na matumaini ya kuwepo
kwenye msafara huo.
Mastaa hao wanne ambao Lechantre hakuwajumuisha ni pamoja na kiungo
mkongwe, Mwinyi Kazimoto, mabeki wa pembeni, Jamali Mwambeleko na Ally
Shomary, Kipa Emmanuel Mseja na kiungo mshambuliaji Mohammed Ibrahim
‘MO’ waliobaki jijini Dar.
Wachezaji hao ambao walitemwa wanaungana na waliotoka majeruhi akiwamo
Haruna Niyonzima na Salum Mbonde ambao wanaendelea kukusanya nguvu kabla
ya kuanza kupewa majukumu katika mechi zilizosalia za VPL.
Wachezaji wao walikuwa na matumaini ya kuambatana na timu kutokana na
mazoezi makali waliyopiga mara ya mwisho juzi jioni kabla ya timu
kujichimbia kambi ya muda mfupi ya Sea Scape na baadhi yao akiwamo
Mwambeleko amekubali yaishe.
Mwambeleko aliyetua Msimbazi msimu huu akitokea Mbao FC, alisema hana
kauli kwa kuwa maamuzi ya kocha juu ya nan i awepo kikosini ni kocha,
japo alikuwa na hamu ya kuitumikia timu yake katika mechi hiyo ya
ugenini itakayopigwa Jumanne.
“Kwa upande wangu nilikuwa nafanya mazoezi kwa nguvu zote ili Lechantre
aweze kunifikiria, huenda hajaridhishwa na kiwango na sasa naendelea
kujifua mazoezi binafsi ili wakirudi safari niweze kumridhisha mwalimu,
nina hamu ya kuingia kikosini,” alisema.
“Kiukweli nimeumia, ila sina jinsi zaidi ya kupambana zaidi na
kuhakikisha napata nafasi ya kucheza ingawa nafasi ambayo nacheza tupo
wachezaji watatu,” alisema.
OKWI KATISHA
Katika mazoezi ya Simba ambayo walifanya kwa mara ya mwisho juzi Ijumaa
jioni katika uwanja wa Boko Veterans kinara wa mabao wa Ligi Kuu Bara,
Emmanuel Okwi hakuwepo kwa maelezo alikuwa kwao Uganda lakini alitua na
kuwepo katika msafara.
Okwi aliwasili kambini katika Hotel ya Sea Scape usiku wa juzi na jana
aliungana katika msafara na wenzake na kuondoka wote Njombe.
“Kweli hakuwepo mazoezi ya mwisho tuliofanya Dar es Salaam lakini
tulishawasilina nae na aliingia kambini na tupo naye kwenye msafara, ila
sijui kwanini Juuko Murshid alichelewa japo waliondoka wote kwenda
kulitumikia taifa lao,” alisema mmoja wa vigogo wa Simba.
MSIKIE MRUNDI
Kocha Msaidizi wa Simba, Masudi Djuma alisema walikaa na Lechantre
waliona ni vyema kufikia Iringa kwa siku moja ili wachezaji wazoee
mazingira ya baridi na siku inayofuata yaani kesho waingie Njombe kwani
si mbali na hapo. Lengo ni kuhakikisha tunashinda mchezo wetu muhimu.”
- Get link
- X
- Other Apps
- Get link
- X
- Other Apps
Comments