Sitabaki Nilivyo ya Joel Lwaga kusindikiza uzinduzi wa Jimmy D psalmist Jumapili Katika Ukumbi wa King Solomon
MWIMBAJI nyota wa muziki wa injili kutoka nchini Nigeria Jimmy D psalmist tayari
ametua nchini na Jumapili hii ya mwisho wa wiki atazindua ujio wa albamu yake mpya iitwayo
restaurant Namanga Dar es Salaam.
Hayo yamesemwa Jijini hapa na mwandaaji wa onesho hilo la Injili Rose Alphonce'
Muna Lose' amesema kuwa mwimbaji huyo ni yupo katika kiwango cha juu katika uimbaji wa
muziki na kuwa atapanda kuimba katika siku hiyo iliyopewa jina la Mwanzo Mpya.
Amesema Jumla ya waimbaji kama Joel Lwaga anaye fanya vema na wimbo wake mpya uitwao
Sitabaki Nilivyo atakuwa ni mmoja wa waimbaji watakao pamba jukwaa la uzinduzi huo.
"Tiketi zitaanza kuuzwa siku hiyo katika ukumbi huo wa king solomon ambapo
wapendwa wa muziki wa Injili watatakiwa kununua tiketi hizo mapema bila usumbufu,
kwani kuchelewa kununu kunaweza kumsababisha msongamano,"amesema Muna Lose.
Lwaga
Muna Lose amesema kuwa licha ya mwimbaji mahiri Lwaga kupangwa kusapoti kwa nguvu
onesho hilo waimbaji wengine wamuziki huo kama Poul Clement ,
Joel Lwaga
Wengine Upendo Nkone ,Ambwene
Mwasongwe pamoja na Abby Chams watapanda kusapoti onesho hilo ambapo VIP kiingilio
kimepangwa kuwa ni Sh 20,000 huku maeneo ya kawaida yakiwa ni Sh 10,000 ambapo
onesho hilo lililo pewa kauli mbiu ya Mwanzo Mpya limepangwa kuanza saa 9:00
mchana.
Comments