Imeelezawa kuwa nchini Utalii umekuwa ukikua mwaka hadi
mwaka na kuvutia zaidi ya watalii milioni moja laki mbili(1,200,000)
na kuchangia asilimia 17.5 ya pato la uchumi wa Taifa kwa mwaka,
hivyo kushika nafasi ya pili baada ya shughuli za kilimo ambapo
huchangia asilimia zaidi ya asilimia 25.
Hayo yamesemwa leo na Mkurugenzi Mtendaji bodi ya utalii ya
Taifa Devotha Mdachi katika uzindizi wa tamasha la Taaluma
(Career Day) lililo andaliwa na Chuo Cha Utalii Dar es Salaam .
Mkurugenzi Mtendaji bodi ya utalii ya
Taifa Devotha Mdachi katika uzindizi wa tamasha hilo.
Amesema sekta ya Utalii imechangia kuwepo na ajira takribani
540,000 huku idadi ya wataliiinaendelea kuongezeka na matarajio
ya watalii kutoka katika sehemu mbali mbali zinazotoa huduma
zitatakiwa kukidhi viwango vya kimataifa.
"KUkidhi viwango vya kimataifa kunafanya sekta hii kuwa na
uhitaji wa watumishi wenye elimu,weledi na ujuzi stahiki,
na kiuchumi,uchumi wa taifa letu umeendelea kukua kwa
wastani wa asilimia 7 kwa miaka mitano mfululizo,"amesema
Devotha.
Devotha amesema utalii wa dunia pia umeendelea kukua mfululizo
kwa kipindi cha miaks sita na hivyo kuchangia asilimia 10.2
ya uchumi wa dunia kwa dola za kimarekani trioni 7.6 na hivyo
kufanya sekta hiyo kuchachangia ajira milioni mbili
tisini na mbili(Milioni 292) kwa uwiano wa 1:10 za kazi
duniani ambapo sekta hiyo itaendelea kukua kwa asilimia
3.9 kwa mwaka kwa kipindi cha miaka 10 ijayo(World Travel
and TourismCouncil,March 2017).
Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Chuo Cha Taifa
Cha Utalii Dr .Shogo Mlonzi Sedoyeka akizungumza mbele ya wanahabari
mara baada ya kumalizika tamasha hilo.
Kwa upande wake Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Chuo Cha Taifa
Cha Utalii Dr Shogo Mlonzi Sedoyeka amesema kuwa Chuo hicho kimekua
kikichukua wanafunzi mikoa tofauti ambapo wanafunzi wanaotoka
nje ya jiji la Dar es Salaam wamekuwa wakizingatiwa zaidi
kwa kupewa hostel.
"Wanafunzi wanaotoka mikoa mbali mbali nje ya Jiji la Dar
wao tumekuwa tukiwapa nafasi zaidi katika masomo ya
chuoni hapa ambapo wamekuwa wakipatiwa mafunzo ya Ukarimu,
na sekta za utalii,"anasema Dr Sedoyeka.
Dr Sedoyeka anaongeza kusema kuwa chuo kimekuwa kikitoa pia
mafunzo ya muda mfupi na mafunzo ya uitaji maalum, kwa kutumia
mitaala inayofuata mfumo wa kujenga ujuzi.
Anasema chuo hicho kina ithibati kutoka Baraza la Taifa
la Elimu ya Ufundi NACTE) ya kutoa mafunzo ya ukarimu ,
usafilishaji watalii na uongozaji watalii katika ngazi
ya Stashahada na Astashahada.
Comments