Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe
Magufuli amewataka Watanzania kutowasikiliza Wabunge wanaosema serikali
inadaiwa madeni ilhali wao wanapita katika barabara hizo kuelekea
bungeni.
Rais Magufuli ameyasema hayo mjini Iringa alipokuwa akifungua barabara ya Lami ya Iringa – Migoli- Fufu inayounganisha mikoa ya Iringa na Dodoma.
Rais Magufuli ameyasema hayo mjini Iringa alipokuwa akifungua barabara ya Lami ya Iringa – Migoli- Fufu inayounganisha mikoa ya Iringa na Dodoma.
Rais
Magufuli amesema kuwa hata katika ukopaji unaweza ukakopa leo na
ukalipa baada ya miaka 40 au 50 huku akieleza kuwa madeni anayokopa yeye
huenda yakalipwa yeye hayupo duniani.
“Kwahiyo mimi nataka niwaeleze ukweli ndugu zangu, lile deni
walilokopa wakoloni waingereza kwa kujenga ile barabara ya Morogoro Road
kule Dar es salaam deni lake limemalizika mwaka juzi amelimaliza
Kikwete, deni lilikopwa kwaajili ya uhuru kile kipande na si barabara
yote kwahiyo unaweza ukakopa leo ukalipa baada ya miaka labda 40 hata
miaka 50 madeni tunayolipa sasa hivi yanayolipwa yamekopwa katika awamu
hizo zote,“ amesema Rais Magufuli.
“Inawezekana awamu ya madeni ninayo kopa yatalipwa wala mimi sipo
duniani na ndio maana huwa mnawasikia wengine wanazungumza serikali
inadaiwa madeni na huwa wanasahau wengine wanatoka huku Iringa
wanaitumia hiyo hiyo barabara kwenda Bungeni, wanaitumia barabara hiyo
hiyo kwa magari yao waliyoyapata waliyokopeshwa lakini wakiisha fika
kule wanasema serikali inadaiwa madeni wanasahau kuwa hayo madeni ni
pamoja na barabara waliyoipitia wakati wanaenda Bungeni.“
Comments