kodi kutoka TRA, Richardi Kayombo.
Mamlaka ya mapato Nchini Tanzania (TRA), imesema katika miezi tisa ya mwaka wa fedha 2018/17 imekusanya jumla ya shilingi Trilioni 11.78 ikilinganishwa na shilingi Trilioni 10.86 ambazo zilikusanywa kipindi cha mwaka wa fedha wa 2016/17.
Kiasi hicho ni sawa na ukuaji wa asilimia 8.46 ikilingasnisha na trilioni 10.8 zizokusanywa katika kipindi kama hicho katika mwaka uliopita.
Hayo yamesemmwa leo jijini dar es salaam na Mkurugenzi wa huduma na elimu kwa mlipa kodi kutoka TRA, Richardi Kayombo wakati akizungumza na wandishi wa habari amabapo amesema kuwa katika mwezi machi 2018 wamekusanya jumla ya shilingi trilioni 1.54 ikilinganishwa na makusanyo ya mwezi machi 2017 ambapo ilikusanywa shilingi Trilioni 1.34 ambayo ni sawa na ukuaji wa asilimia 14.49.
Aidha amesema kuwa bado usajili wa walipa kodi wapya unaendelea wakiwemo wamachinga ambapo kwa wiki hii wako katika mkoa wa geita
Katika hatua nyingine kayombo amesema kuwa kwa sasa wanacnhi wanaweza kulipa kodi ya majengo kwa njia ya mtandao kwa kumia simu ya mkononi kwa kupiga *152*00# na kufuatiwa na maelezo
Comments