Wanajeshi wa Nigeria wamefanikiwa kuzuia shambulizi la wanamgambo wa Boko Haram katika mji wa kaskazini mashariki wa Maiduguri hapo jana, ikiwa ni tukio la pili la aina hiyo katika mwezi mmoja. Jeshi limesema katika taarifa kuwa wanajeshi wa Operesheni ya Lafiya Dole walifanikiwa kuzima shambulizi la Boko Haram viungani mwa eneo la Jidari Polo la mji wa Maiduguri.
Milipuko na milio ya risasi ilisikika na wakaazi wa mji huo ambao ndio mji mkuu wa Borno, jimbo lililoathirika zaidi na uasi wa kundi hilo. Wanamgambo wa kundi hilo walijaribu kuingia Maiduguri mapema mwezi huu, huku wakipigana na wanajeshi katika shambulizi ambalo karibu watu 15 waliuawa na 83 wakajeruhiwa. Rais Muhammadu Buhari, aliyeingia madarakani mwaka wa 2015 akiapa kuumaliza uasi huo, amelipa kipaumbele suala la kuimarisha usalama nchini humo. Suala hilo linatumika sana kisiasa wakati nchi hiyo ikijiandaa kwa uchaguzi mwaka ujao ambao Buhari amesema atagombea
.
Comments