Maya Magimba Afisa Msaidizi wa Huduma kwa mlipa Kodi kutoka Mamlaka ya Mapato (TRA)akitoa mada katika moja mwaka jana.
Mamlaka ya Mapato Tanzania imeendelea kusisitiza umma wa Watanzania na
wafanyabiashara kwa ujumla kutumiashine za EFD,huku ikisisitiza kuwa Mtu
binafsi awe mkazi au si mkazi anatakiwa kutembelea ofisi ya TRA ya mkoa
au wilaya na kujaza fomu ya maombi ya Namba ya Utambulisho wa Mlipakodi
(TIN).
Mkuu
wa Wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam Felix Lyaniva (mwenye sharti
la mikono mirefu),akikata utepe katika mfao wa cheti ikiwa ni kuashiria
kuanza kwa tukio la utoaji vyeti vya kutambua viwanda vidog vidogo 300
jijini.Vyeti hivyo vimetolewa na Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogo
vidogo(SIDO).
Hayo yamesemwa na Maya Magimba ambaye ni Afisa huduma kwa mlipakodi
wakati Shirika la kuhudumia Viwanda Vidogo vidogo(SIDO),likikabidhi
vyeti vya kutambua viwanda vidogo vidogo na vya kati kwa
wamiliki na wajasiriamali zaidi ya 300 kwa Mkoa wa Dar es Salaam.
Tukio la utoaji vyeti lilifanyika sikuchache zilizopita Jijini Dar es Salaam
ambapo aliekabidhi vyeti vya kuwatambua wamiliki na wajasiriamali
wa viwanda hivyo alikuwa ni Mkuu wa Wilaya ya Temeke Felix Lyaniva
kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa Paul Makonda ambaye alipaswa kuwa mgeni rasmi.
"Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) inapenda kuwahakikishia Wafanyabiashara
na Watanzania kwa ujumla kuwa utaratibu wa kutumia Mashine za EFD ulianzishwa
kwa lengo la kumrahisishia mfanyabiashara utunzaji wa kumbukumbu
za biashara za kila siku pamoja na kuondoa usumbufu wakati wa
ukadiriaji wa kodi,"alisema Magimba.
Magimba alisema kuwa Hati ya kwanza unayopaswa kupewa na
TRA ni namba ya utambulisho ya mlipakodi (TIN),nakuwa ni wajibu
wa mfanyabiashara kulipa kodi kwa wakati na kuwa mteja anaweza
kupiga namba za kituo cha huduma kwa mlipa kodi 080075
ambapo kupiga namba hiyo ni bure huku mwisho wa kupiga ikiwa
ni saa 2:00 usiku.
Kupitia tukio la utoaji vyeti imelezwa kuwa kuna wajasiriamali
600 na kati yao ndio hao wamepewa vyeti ili kutambua viwanda vyao
na mchango wao katika jitihada za kuleta maendeleo kuelekea Serikali
ya viwanda nchini.
Mamia yaWajasiriamali wa Jjiji la Dar es Salaam waliweza kufika
wa mkoa huo, Mkuu wa Wilaya ya Temeke Lyaniva akisema SIDO wamefanya
tukio la kihistoria kwa kutambua mchango wa wamiliki wa viwanda hivyo
na kuongeza Serikali kwa upande wake itazifanyia kazi changamoto za
wajasiriamali hao.
"Natoa pongezi na shukrani kwa Mkurugenzi Mkuu wa SIDO kwa kuendelea
na majukumu yao ya kuwasimamia wajasiriamali wadogo na wakati
ili watimize malengo yao,"alisema Lyaniva.
Comments