Liverpool imefanya maangamizi kwa Manchester City katika robo fainali ya Champions League baada ya kuwachapa vinara hao wa Premier League 3-0.
Manchester City inahitaji miujiza katika mchezo wa marudiano utakaofanyika Etihad Stadium ili kutinga hatua ya nusu fainali.
Kwa mtazamo mwepesi ni kama vile Manchester City wameshatanguliza mguu mmoja nje baada ya kuruhusu magoli ya haraka haraka kutoka kwa Mohamed Salah, Mohamed Salah na Mohamed Salah katika dakika ya 12, 21 na 31.
Kocha wa Manchester City, Pep Guardiola amekiri kuwa wana mlima mrefu wa kupanda, lakini watajaribu kupambana hadi sekunde ya mwisho.
“Tulicheza vibaya kipindi cha kwanza na tukaadhibiwa. Tunajua tuna kazi ngumu katika mchezo wa marudiano, ila tutajaribu kupata matokeo mazuri”, alisema Guaridola wakati akihojiwa baada ya mchezo kumalizika.
Comments