.
Jina Langu ni
Valence niliweza kukutana na shirika la vijana IYF mwaka 2013 na kuanza maisha
ya kujitolea mwaka 2014 baada ya kuhudhurio kambi ndogo ya kubadilisha.
Fikra hivyo
kupitia wakati huo nilivutiwa sana na shirika hili na kutaka kujifunza lugha tu,
Lakini kulingana na elimu na mafunzo niliyopata kupitia kambi mbali mbali
niliamua kutafuta fursa ya kua mtuwa kujitolea ng'ambo na kufani kiwa kwenda
Amerika ya kusini Paraguay na kukaa kule mwaka mmoja.
Katika kipindi
changu cha kujitolea nchini Paraguay niliweza kujifunza mambo mengi ambayo
sikua nikiyafahamu ikiwepo lugha ya Kispanishi, pia kuhusu elimu ya ufahamu
lakini kubwa zaidi ikiwa ni pamoja na elimu ya moyo, hapa niliweza kukumbana na
changamoto mbali mbali lakini changamoto kubwa ikiwa ni chakula na tamaduni za
kule, mwanzo sikuwahi kula nyama lakini kupitia maisha yale niliweza kubadili
mtizamo na kuzoea chakula cha kule.
Valence
Pia kupitia
maisha yangu ya kujitorea nje imenifanya kuwajibika na kujitolea kijamil kwani
maisha yale yalikua magumu sana kwangu.
Mwanzoni sikua
nikijua kuongea lugha vizuri pia sikua na uhuru wa kujielezea nlikua naogopa
sana kushiriki na wenzangu kuhusu kipaji nilichonacho lakini niliweza kufungua
moyo na kujifunza vyema.
Faida: Hakika
nilikua mwenye bahati na neema kupata nafasi ya kujitolea ng'ambo kwani
niliweza kufundisha lugha ya Kiswahili na kueleza utamaduni wa kiafrika.
Pia
nilifundishwa kuhusu elimu ya ufahamu na moyo na kufundisha watu mbali mbali
wenye mawazo hasi kuhusu mtizamo wa maisha.
Utamaduni:
katika utamaduni wa nchi niliyokwenda ilikua ni tofauti na Tanzania mwanzoni
nilishindwa kuelewa utamaduni wa kule na kupata changamoto mbali mbali Lakini
nashukuru kushiliki kwangu na watu mbali mbali kulinipa nafasi ya kufundishwa
tamaduni za kule
Kukata tamaa:
kweli kuna wakati nilikata tamaa kwa sababu mlihisi nadharaulika na mambo mengi
siyaelewi ikiwepo lugha lakini yale yalikua ni mawazo yangu, hakika watu
walinipa nafasi ya kutambua kua nchi ile ni ya upendo kwa kunifundisha mambo
mbali mbali.
Mabadiliko: Hii
naamini imenibadili fikra na mtazamo wangu kwani sikuwahi kufikiri ninaweza
kuzungumza lugha zaidi ya mbili pia kupitia wakati ule nilijifunza hata pia
kula vyakula ilikua ni kama muujiza kwani zaidi ya miaka 23 sikuwahi kula nyama
yoyote ile.
Faida: Hii
kweli ni ajabu kwani nilijifunza mambo mbali mbali kuhusu ufahamu na kuweza
kupokea mawazo ya watu wengine, kwamba ili uweze kuelewa lazima ufungue moyo
wako ndipo utaweza kupokea kitu au jambo.
Hivyo kupitia
hii sasa naweza kufundisha lugha ya Spanishi kwa watu wengine na kubadili
mitizamo yetu kua pamoja bila kushurutishwa.
Lengo:
Kuhamasisha vijana wenzangu ili waweze kubadili mitizamo yao kuhusu ufahamu na
mtizamo kwani maisha ya kujitolea ni hamasa kubwa kwa taifa na jamii yetu.
Comments