Na Francis Peter
KITUO cha Uwekezaji nchini (TIC) kimesema kuwa sera nzuri za serikali
ya awamu ya tano, inayoongozwa na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania DKT. John
Pombe Magufuli ambapo zimekuwa kichocheo cha wanaotaka kuja kuwekeza nchini
huku chama cha wafanya biashara cha Ujerumani (DIHK) kikiwa kimefika
nchini kutokana na kuvutiwa na sera hizo.
Mkurugenzi wa Kituo cha Uwekezaji Geoffrey Mwambe
Hayo yalisemwa jana wakati
wa Mkutano na ujumbe wa Wawekezaji hao, waliotoka nchini Ujerumani
kwenye mipango ya kuja kuwekeza nchini.
Alisema chama hicho cha DIHK kikiwa kimeongozwa na Mkurugenzi wao
Dr Martin Wansleben kimesema kimevutiwa na sera nzuri na kuwa
kikpo tayari kuwekeza nchini.
"Ujembe wa nchini hiyo ulifika na tumeweza kujadiliana na hoja mbali mbali
juu ya wao kuwekeza nchini ambapo hiyo ni mara ya pili sasa Wajerumani
kutua nchini katika jambo hilo linalovutiwa na sera ya nzuri za serikali
ya awamu ya tano,"alisema Mwambe.
Mwambe alisema kuwa mkutano huo ulikuwa na hoja mbali mbali na kuwa
wageni hao waliweza kudadisi zaidi masuala mbali mbali kama suala
la mihundo mbinu namambo mengine kama ukuaji wa idadi ya watu kwa
kila mwaka jambo ambalo ni la msingi kwa mwekezaji kulifahamu katika
kipindi hiki .
Aidha Mkurugenzi wa DIHK alisema kuwa tayari wao wanataka kuwekeza
Afrika nakuwa tayari wamekubali kufungua ofisi zao nchini Tanzania
huku ikiwa ni moja ya mafanikio hayo yanayotazamiwa kuwa bora nchini.
"Nimeridhishwa na mazingira bora kabisa kibiashara na hivyo tumeamua kuja
nchini Tanzania kwa nia moja ya uwekezaji kibiashara na kuwa tunaomba
kupewa ushirikiano wa kutosha na taasisi mbali mbali za serikali
na zisizoza serikali pamoja na makampuni mengine ya Tanzania,"alisema
Dr Martin.
Dr Martin alisema kuwa ameambatana na viongozi wengine wa serikali pamoja
na wawekezaji na wabunge wa Ujerumani katika mkutano huo na kuongeza
kuwa ushirikiano utasababisha hatua za kiuchumi kukua kwa haraka.
TIC katika mkutano na wamekezaji hao ilipambanua kuwa hukuaji wa ongezeko la
watu nchini ni asilimia 2.7 kwa mwaka ambapo ni kichocheo kingine kinachoweza
kumvutia mwekezaji.
Comments