Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda(picha na mtandao)
Na Mwandishi wetu Dar es salaam
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda ametoa rai walimu wakuu na hasa kwa Ofisa Elimu Mkoa wa Dar es Salaam kuwapa taarifa walimu wa shule zote kuwa kwa siku mbili hizi Jumanne na Jumatano wanafunzi wasiende shuleni.
Mkuu wa Mkoa Makonda ameyasema hayo jijini Dar es salaam kufuatia mvua zinazoendelea kunyesha ambapo ameelza kuwa zimesababisha maafa kwa kufariki watu nane kutoka na mvua hizo.
RC Makonda amesema vifo hivyo vimetokana na mafuriko katika baadhi ya maeneo ya Jiji la Dar es Salaam ambapo ameeleza ipo haja ya wakazi wa Jiji hilo kuhakikisha wanakuwa makini katika kipindi hiki ambacho mvua zinaendelea kunyesha.
tazama video chini na usubscribe uone namna ambavyo mvua zimeleta athari kwa makazi ya watu .
tazama video chini na usubscribe uone namna ambavyo mvua zimeleta athari kwa makazi ya watu .
Comments