Kenneth Stanley Njindo Matiba kwa sasa ni Marehemu
Ken, kama alivyojulikana nchini Kenya ameaga dunia katika Hospitali moja ya kibinafsi ya Karen, iliyoko Jijini Nairobi.
Ken Matiba ambaye ni maarufu katika siasa za ukombozi wa pili wa kisiasa nchini Kenya, baada ya ile ya Uhuru miaka ya 1950s na 1960s.
Mwanasiasa huyo maarufu ambaye alitatiza pakubwa siasa za Rais wa awamu ya pili nchini humo mzee Daniel Toroitich Arap Moi, alizaliwa Juni Mosi mwaka 1932 - na akafariki Jumapili April 15 ya mwaka huu wa 2018.BBC
Comments