Manchester United imejiweka kwenye mazingira mazuri ya kumaliza katika nafasi ya pili kwenye Ligi Kuu ya England baada ya kuichapa Bournemouth 2-0 huku Paul Pogba akiwa nyota wa mchezo.
Bao la kwanza la United lilifungwa na Chris Smalling dakika ya 28 baada ya kazi nzuri ya Pogba, Herreira na Lingard.
Lakini ni bao la pili lililowekwa wavuni na Romelu Lukaku dakika ya 70 ndilo lililosisimua zaidi hususan kwa ile juhudi binafsi iliyofanywa na Pogba.
Pogba ambaye aling’ara sana, alichukua mpira mbele kidogo ya box la 18 ya United na kukimbia nao hadi jirani na lango la Bournemouth kabla ya kutoa pasi maridadi kwa mfungaji.
Hii inakuwa mara ya pili ndani ya mechi tatu za mwisho za Premier League kwa Pogba kutajwa kama nyota wa mchezo (Man of The Match). Ya kwanza ilikuwa dhidi ya Manchester City.
Bournemouth (4-4-1-1): Begovic 5.5; Francis 6, S Cook 5.5, Ake 7, Daniels 5..5; Fraser 6, L Cook 6.5, Surman 6 (Gosling 75, 6), Ibe 5.5 (Mousset 56, 6); King 5 (Defoe 82); Wilson 5.5
Manchester United (4-3-3): De Gea 6.5; Darmian 6, Smalling 7, Jones 7, Shaw 6; Fellaini 5, Herrera 7.5 (Matic 72, 6), Pogba 7 (Blind 80); Lingard 6.5 (Lukaku 62, 6.5), Rashford 7, Martial 6.5
Comments