Skip to main content

Posts

Showing posts from April, 2018

Waziri wa Afya Ummy Mwalimu ampatano Alikiba

Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu amemshukuru msanii wa Muziki, Ali Kiba pamoja na mdogo wake, Abdu Kiba kwa kumualika katika sherehe yao baada ya kufunga ndoa. Waziri Ummy amewatakia maisha mema yenye heri, furaha, baraka na maelewano pamoja na wake zao. “ Asanteni sana @OfficialAliKiba na Abdu Kiba kwa kunialika kushiriki nanyi katika Siku yenu. Ninawatakia maisha ya ndoa yenye heri, furaha, baraka na maelewano pamoja na wake zenu Amina na Ruwayda. Hongereni sana ,“ ameandika Ummy leo April,30 kupitia mtandao wake wa Kijamii.

Amber Rudd ametangaza kijiuzulu jana

Amber Rudd Waziri wa mambo ya ndani wa Uingereza  ametangaza kijiuzulu hapo jana Jumapili kufuatia kashifa dhidi ya maafisa wa nchi hiyo kuwahusisha kimakosa wahamiaji kutoka nchi za Carribean na sehemu ya mchakato wa kuwaondoa wahamiaji wanaoishi nchini humo kinyume cha sheria. Waziri Mkuu Theresa May amekubali kujiuzulu kwa Amber Rudd ambaye amekuwa akishinikizwa na chama cha Labor kujiuzulu alikuwa akitarajia kutoa maelezo bungeni leo Jumatatu kuhusiana na kashifa hiyo iliyogonga vichwa vya habari nchini Uingereza kwa siku kadhaa. Kashifa hiyo inafuatia gazeti la Guardian kuripoti kuwa baadhi ya watu waliohamia Uingereza wakitokea nchi za Carribean miongo kadhaa iliyopita baada ya vita kuu vya pili vya dunia wanatishiwa kufukuzwa kutokana na kutowasilisha nyaraka zinazothibitisha kuwa wana haki ya kuendelea kusalia nchini humo.

Rais Dkt. John Pombe Magufuli fungua barabara ya Lami ya Iringa – Migoli- Fufu

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amewataka Watanzania kutowasikiliza Wabunge wanaosema serikali inadaiwa madeni ilhali wao wanapita katika barabara hizo kuelekea bungeni. Rais Magufuli ameyasema hayo mjini Iringa alipokuwa akifungua barabara ya Lami ya Iringa – Migoli- Fufu inayounganisha mikoa ya Iringa na Dodoma.   Rais Magufuli amesema kuwa hata katika ukopaji unaweza ukakopa leo na ukalipa baada ya miaka 40 au 50 huku akieleza kuwa madeni anayokopa yeye huenda yakalipwa yeye hayupo duniani. “Kwahiyo mimi nataka niwaeleze ukweli ndugu zangu, lile deni walilokopa wakoloni waingereza kwa kujenga ile barabara ya Morogoro Road kule Dar es salaam deni lake limemalizika mwaka juzi amelimaliza Kikwete, deni lilikopwa kwaajili ya uhuru kile kipande na si barabara yote kwahiyo unaweza ukakopa leo ukalipa baada ya miaka labda 40 hata miaka 50 madeni tunayolipa sas...

Akina mama na Vijana Manispaa ya Ubungo kupatiwa bilioni 1.9 kwaajili ya mikopo

Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo Jijini Dar es Salaam imetangaza kutoa kiasi cha shilingi bilioni 1.9 kwa ajili mikopo kwa kinamama na vijana na walemavu kuanzia leo . Mgeni rasmi Naibu Waziri wa Nchi ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na serikali za mitaa TAMISEMI Joseph Kakunda aliye katikati  na upande  wa kulia ni Meyawa Manispaa ya Ubungo Boniface Jacob, na upande wa  kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Kisare Makori. Hayo yamesemwa na mgeni rasmi Naibu Waziri wa Nchi ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na serikali za mitaa TAMISEMI Joseph Kakunda katika uzinduzi wa mikopo hiyo viwanja vya Barafu Mburahati. Vviongozi wa CCM Ubungo wakiongozwa na Katibu wao Lucas Magonja wakifurahia wimbo wa kulipongeza Manispaa ya Ubungo ulioimbwa na kikundi cha kwaya cha Wilaya hiyo Alisema ameishukuru Manispaa ya Ubungo kwa kutekeleza vyema Ilani ya CCM  kwa kutenga fedha kwa ajili ya makundi ya  Wanawake, vijana na walemavu, na kumuagiza Katibu...

Kiungo Haruna Niyonzima kuikosa Yanga

KIUNGO wa Simba Mnyarwanda Haruna Niyonzima 'Fabregas'  huenda akaukosa mchezo wao wa Aprili 29 dhidi ya watani wao Yanga  kutokana na kufiwa na dada yake anayeitwa Sumaye kwao Rwanda. Niyonzima ambaye leo mchana imembidi asafiri kurudi Dar es Salaam akitokea Morogoro ambako kikosi chao  cha Simba  kimeweka kambi kwa ajili ya mchezo huo na alitarajia kuondoka  mchana. "Nimepata matatizo bwana, nimefiwa na dada yangu nyumbani Rwanda na hivi sasa niko hapa nyumbani nikijiandaa kwa ajili ya safari. Kwa sababu ni jambo la kushtukiza ndiyo nahangaikia ndege kuona kama naweza kuondoka,"anasema Niyonzima aliyesajiliwa msimu huu akitokea Yanga. Simba na Yanga zinacheza wikiendi hii ambapo kama Niyonzima ataondoka kuna uwezekano mkubwa wa kuukosa mchezo huo ambao kwa kawaida huwa na ushindani mkubwa.

Dkt. Tulia Ackson azungumza na wanafunzi wa vyuo na sekondari

NAIBU Spika  wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson leo amewahasa wanafunzi wa elimu ya juu pamoja na wanafunzi wa shule za sekondari kujituma katika masomo yao kwa kuzingatia malengo sahihi masomoni.  Dkt. Tulia Naibu Spika  wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayo ameyasema ndani ya ukumbi wa Nkrumah wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na   Dkt. Tulia wakati uzinduz rasmi wa programu maalumu inayohusu maisha ya wanafunzi  vyuoni (University Life Campus) maarufu kama UNILIFE CAMPUS. Alisema kawaida ya mtu mwenye uwezo dhidi ya mwengine ni yule anaye jituma hivyo mwanafunzi anatakiwa awena bidii katika masomo na katika hatua zingine za mazingira anayoishi. "Mkizingatia nidhamu ni dhahili mtakuwa umefikiria zaidi muda kwani ukiweza kupangilia na kwendana na muda mambo mengi yatakuwa yameendana na wakati, na pia wasifanye shughuli nyingine ambayo aihusiani na muda huo waliojipangia," a...

Wenger :Hana mpango wa wa kupendekeza atakayerithi mikoba yake Emirates

Kocha Arsene Wenger aliyetanganza kung’atuka Arsenal, amesema hana mpango wa kupendekeza mtu atakayerithi mikoba yake Emirates. Akiongea kwenye mkutano wa waandishi wa habari kuelekea mchezo wa Europa League kati ya Arsenal na Atletico Madrid, Wenger pia alifichua kuwa kutangaza kwake kuondoka Arsenal hakukuja kwa utashi wake bali ni kwa msukumo wa bodi. “Sina mpango wa kupendekeza mrithi wangu. Kwasasa sitaki kuzungumza lolote juu ya hilo,” alisema Wenger baada ya kuulizwa iwapo atapendekeza kocha mpya Arsenal.

Shambulizi La Boko Haram Lazimwa Nigeria

Wanajeshi wa Nigeria wamefanikiwa kuzuia shambulizi la wanamgambo wa Boko Haram katika mji wa kaskazini mashariki wa Maiduguri hapo jana, ikiwa ni tukio la pili la aina hiyo katika mwezi mmoja. Jeshi limesema katika taarifa kuwa wanajeshi wa Operesheni ya Lafiya Dole walifanikiwa kuzima shambulizi la Boko Haram viungani mwa eneo la Jidari Polo la mji wa Maiduguri. Milipuko na milio ya risasi ilisikika na wakaazi wa mji huo ambao ndio mji mkuu wa Borno, jimbo lililoathirika zaidi na uasi wa kundi hilo. Wanamgambo wa kundi hilo walijaribu kuingia Maiduguri mapema mwezi huu, huku wakipigana na wanajeshi katika shambulizi ambalo karibu watu 15 waliuawa na 83 wakajeruhiwa. Rais Muhammadu Buhari, aliyeingia madarakani mwaka wa 2015 akiapa kuumaliza uasi huo, amelipa kipaumbele suala la kuimarisha usalama nchini humo. Suala hilo linatumika sana kisiasa wakati nchi hiyo ikijiandaa kwa uchaguzi mwaka ujao ambao Buhari amesema atagombea .

Devotha Mdachi :Azindua Tamasha Chuo cha Utalii

Imeelezawa kuwa nchini  Utalii umekuwa ukikua mwaka hadi  mwaka na kuvutia zaidi ya watalii milioni moja laki mbili(1,200,000) na kuchangia asilimia 17.5 ya pato la uchumi wa Taifa kwa mwaka, hivyo kushika nafasi ya pili baada ya shughuli za kilimo ambapo huchangia asilimia zaidi ya asilimia 25. Hayo yamesemwa leo na Mkurugenzi Mtendaji bodi ya utalii ya  Taifa Devotha Mdachi katika uzindizi wa tamasha la Taaluma  (Career Day) lililo andaliwa na Chuo Cha Utalii Dar es Salaam .  Mkurugenzi Mtendaji bodi ya utalii ya  Taifa Devotha Mdachi katika uzindizi wa tamasha hilo. Amesema sekta ya Utalii imechangia kuwepo na ajira takribani 540,000 huku idadi ya wataliiinaendelea kuongezeka na matarajio ya watalii kutoka katika sehemu mbali mbali zinazotoa huduma zitatakiwa kukidhi viwango vya kimataifa. "KUkidhi viwango vya kimataifa kunafanya sekta hii kuwa na uhitaji wa watumishi wenye elimu,weledi na ujuzi stahiki, na ...

Mchezaji wa Klabu ya Liverpool Salah Ashinda Tuzo Nyingine Tena.

Mohamed Salah Mchezaji wa Klabu ya Liverpool ameshinda tuzo ya mchezaji bora wa kiume wa mwaka inayotolewa na Shirikisho la wachezji wa kulipwa nchini Uingereza, Proffessional Footballers Association (PFA). Hii ni tuzo nyingine tena baada ya kushinda Tuzo ya mchezaji bora wa Afrika anaechezea ligi ya nje ya Afrika iliyotolewa na BBC, lakini pia ni baada ya kuibuka mchezaji bora wa EPL kwa mwezi March. Katika tuzo hiyo, Salah anaweka rekodi ya kuwa mchezaji wa kwanza raia wa Misri na mchezaji wa 7 wa Liverpool kushinda tuzo hiyo, ambapo tuzo hiyo imekuwa ikiwaniwa na wechezaji wengi na wakubwa katika soka duniani akiwemo, Harry Kane wa Tottenham Hotspur, David De Gea, Golikipa wa Manchester United, Kevin De Bryune, David Silva na Leroy Sane viungo washumbuliaji wa mabingwa wa Ligi kuu England Manchester City. Naye Leroy Sane amejishindia tuzo ya mchezaji bora chipukizi wa soka nchini Uingereza na kuwashinda  Sterling wa Man City na Marcus Rashford wa Manchester Un...

Ajari ya gari yaua watu 10

Polisi mjini Toronto nchini Kanada wamethibitisha kuwa watu 10 wameuwawa baada ya dereva wa gari kuwagonga kwa kudhamiria. Katika tukio hilo Watu wengine 15 wameripotiwa kujeruhiwa, ambapo taarifa kutoka hospitali ya Sunnybrook iliyopo katika mji huo zimefahamisha kwamba baadhi ya majeruhi wapo katika hali mbaya. Dereva wa gari hilo alijaribu kukimbia lakini polisi walifanikiwa kumkamata. Kaimu mkuu wa polisi wa Toronto Peter Yuen amesema dereva huyo anachunguzwa na ametoa mwito kwa walioshuhudia tukio hilo kujitokeza na kutoa taarifa zaidi .

Marenga Millers waelezea Wajasiriamali ufugaji wa tija

IMEELEZWA chakula bora  kwa Nguruwe ni moja ya suala muhimu kwenye dhana nzima ya ufugaji wa nguruwe wenye tija na faida kwa mfugaji kwa sababu kinagharimu kama asilimia 70 ya gharama zote za ufugaji. Hayo yalisemwa Dar es Salaam juzi na Shanel John ambaye ni msemaji wa kampuni ya  Marenga Animal Feeds wakati wa semina yenyekulenga kutoa fursa kwa wadau. Marenga organized a seminar on getting better profit on your layers and your broilers! Everything you need to profit your birds is included in the feed vision! Alisema Lishe duni ni kati ya matatizo mengi yanayosababishwa ukosefu wa tija na ufanisi duni wa uazilishaji wa nguruwe lakini nguruwe wakipatiwa lishe bora,tija na ufanisi wa uzali shaji utakuwa mkubwa hivyo kuongeza faida kwa mfugaji. "kwa mkulima akiwa na mbegu bora ya nguruwe watoto wanakuwa tayari kuachishwa kunyonya baada ya mwezi mmoja na hivyo kumwezesha nguruwe kupata tena joto siku ya tano baada ya kuachishw...

Taarifa kwa vyombo vya habari

Watani wa Jadi wakutana Mmoro

KIKOSI cha Yanga kinatarajia kuwafuata watani zao Simba ambao wako mkoani Morogoro tangu juzi kwa ajili ya kujiandaa na mchezo wa marudiano wa Ligi Kuu Tanzania Bara utakaopigwa Jumapili kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Simba iliwasili Morogoro ikitokea Iringa baada ya mechi yake dhidi ya Lipuli FC wakati Yanga wametua mkoani humo jana baada ya kulazimishwa sare ya bao 1-1 na Mbeya City jijini Mbeya. Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Simba, Haji Manara, alisema kuwa timu yao imeweka kambi Morogoro na wanaamini ni mahali sahihi kwa lengo la kuwajenga wachezaji wake kuelekea mchezo huo wa Jumapili. "Timu iko Morogoro, hali ya hewa na mazingira ya kambi ni rafiki, tunaamini benchi la ufundi litapata kile ilichokihitaji kuelekea mchezo wetu dhidi ya watani zetu," alisema Manara. Naye Meneja wa Yanga, Hafidh Saleh, alisema kuwa kikosi cha Yanga kilitarajiwa kuwasili Morogoro jana jioni tayari kuanza mazoezi ya kuwavaa watani zao. ...

Kanisa lashambuliwa Nigeria zaidi ya watu 10 wameripotiwa kufa

Mapadri wawili wa kanisa Katoliki na waumini 16 wa kanisa hilo waliuawa katika shambulizi lililotokea katika kijiji cha Mbalom katika jimbo la Benue, nchini Nigeria.  Shambulizi hilo lililotokea katikati mwa nchi ambako kumeendelea kushuhudiwa mapigano ya kikabila limehusishwa wafugaji waliokua waibebelea silaha. Mashahidi wanasem ashambulizi hilo lilitokea mapena Jumanne asubuhi Aprili 24. Washambuliaji hao waliingia katika kanisa wakati wa sherehe ya mazishi katika kijiji cha Mbalom, katika jimbo la Benue, nchini Nigeria. Mapadri wawili na waumini 16 wa kanisa Katoliki, wote waliuawa kwa kupigwa risasi, kwa mujibu wa mashahidi walionukuliwa na shirika la habari la AFP ambao pia wamesema watu wengi walijeruhiwa. Washambuliaji pia walipora katika zaidi ya nyumba 60 na katika maduka ya chakula. Wakazi walikimbilia katika viijiji jirani kwa kuhofia usalama wao. Dayosisi ya Makurdi, mji mkuu wa Jimbo la Benue, imelaani vurugu ambazo zilikumba mojawapo ya makanisa y...

Msanii Jebby aliyefanya kweli na ngoma yake Swahiba amefariki dunia

 April 22,2018 wakati wasanii na wadau mbalimbali wakiwa wamejitokeza wenye viwanja vya leader Club jijini Dar es salaam kuuaga mwili wa Video queen Masogange,imeelezwa kuwa Msanii wa bongo fleva anayefahamika kwa jina la Jebby ambaye amewahi kufanya vyema na wimbo kama Swahiba amefariki dunia leo mjini Dodoma alipokuwa akipatiwa matiba Watu wa karibu na msanii Jebby wamesema kuwa msanii huyo alikuwa anaumwa na mpaka umauti umemkuta Dodoma alikuwa akisumbuliwa na matatizo ya bandama na ndiyo yaliyosababisha kifo chake.  bofya chini usikilize moja kati ya Nyimbo ambayoenzi za uhai wake ilimtambulisha vyema kwenye tasnia ya muziki wa bongo flavour

CHUO CHA TAIFA CHA UTALII CHAANDAA SIKU YA TAALUMA

Kaimu Mkurugenzi wa Mafunzo na shughuli za kitaalam katika chuo hicho,Stephen Madenge akizungumzia kuelekea  siku ya taalum. Ili kuendelea kukuza ukuzaji wa sekta ya utalii na ajira nchini,Chuo  cha Taifa cha Utalii kimeandaa tamasha la siku ya taaluma lenye ujumbe  wa fursa za Ajira kwa vijana kupitia taaluma ya Ukarimu na utalii. Hayo yameelezwa leo na Kaimu Mkurugenzi wa Mafunzo na shughuli za  kitaalam katika chuo hicho,Stephen Madenge wakati akikzungumza na  waandishi wa habari jijini Dar es salaam,ambapo amesema lengo ni  kuhakikisha wanawaleta wadau mbalimbali karibu kupitia sekta ya utalii. Magenge amesema sekta ya utalii nchini haijapungua kwani imeendelea kufanya  vizuri kwa kuweza  kujipatia watalii ukilinganisha na nchi zinazozunguka  Afrika Mashariki hivyo wataendelea kutoa elimu ya utalii kwa watanzania. "Kwa kutumia tamasha hili wanafunzi wataonesha kwa vitendo uhodari wa taaluma  zitol...

Nyota wa muziki wa Bongoflava Ali Kiba na Diamondi wakutana kwenye msiba wa Masogange

Diamond Platnum aliyevalia suti nyeusi akimpa mkono Alikiba aliyevalia kanzu nyeupe   Aprili 22, 2018 kwenye viwanja vya Leaders jijini Dar es salaam wasanii na wadau mbalimbali nchini wamejumuika kwa pamoja kuuagaa mwili wa Muigizaji wa filamu na Video Vixen, Agness Gerald Masogange ambaye amefariki dunia siku ya juzi. Licha ya wasanii wengi kujitokeza kumeibuka kelele kwenye msiba huo mara baada ya mahasimu wawili wa muziki wa Bongo flavor Tanzania Alikiba pamoja Diamond Plutnumz mara baada ya kupeana mikono. Katika msiba huo Msanii Alikiba amezungumza mengi ikiwemo na kuwashauri wasanii wenzake katika suala zimala kufikiria kuwa kifo kipo hivyo ni vyema kila msanii akafanya maandalizi sahihi “Nachopenda kuwaambia kila mmoja wenu tufanye yote ambayo tunaona ni muhimu hapa duniani lakini tumkumbuke Mwenyezimungu lazima akumbukwe kila wakati”Amesema Alikiba wakati akitoa hotuba yake kwenye msiba Kwa upande wake Msanii Diamond Platnumz amesema Marehemu Maso...

Jamii yatakiwa kuonesha upendo kwa watoto

Naibu waziri wa afya, jinsia wazee na watoto Dkt, Faustin Ndugulile ameitaka jamii kuonyeshwa upendo na mapenzi mema watoto walio na ugonjwa wa usonji kwani no wana haki ya kupatiwa malezi bora kama watoto wengine. Ameyasema hayo  wakati akizungumza na kituo kimoja cha redio Mkoani Dodoma  ambapo amedai kuwa ugonjwa huo unawapata watoto wadogo na ni ugonjwa unaohitaji watoto kuonyeshwa upendo pamoja na kuwajengea uwezo ili waweze kuwa raia wazuri wa baadae. Akizungumzia ugonjwa huo DKT Ndugulile amesema ugonjwa huo hauna tiba huku akidai kuwa dalili za ugonjwa huo hubainika pale mtoto anapokuwa na mwaka mmoja au zaidi na moja ya dalili hizo ni pamoja na kushindwa kuongea. Hata hivyo  Ndugulile amesema serikali inatambua uwepo wa ugonjwa huo na tayari hatua zimeanza kuchukuliwa ikiwa ni pamoja na kutoa elimu kwa walimu ili kuyafahamu makundi ya watoto hao hali itakayosaidia kuyatambua mahitaji maalum yanayopaswa kutolewa kwa watoto hao. S...

Angalia kazi nzuri ya Pogba

Manchester United imejiweka kwenye mazingira mazuri ya kumaliza katika nafasi ya pili kwenye Ligi Kuu ya England baada ya kuichapa Bournemouth 2-0 huku Paul Pogba akiwa nyota wa mchezo. Bao la kwanza la United lilifungwa na Chris Smalling dakika ya 28 baada ya kazi nzuri ya Pogba, Herreira na Lingard. Lakini ni bao la pili lililowekwa wavuni na Romelu Lukaku dakika ya 70 ndilo lililosisimua zaidi hususan kwa ile juhudi binafsi iliyofanywa na Pogba. Pogba ambaye aling’ara sana, alichukua mpira mbele kidogo ya box la 18 ya United na kukimbia nao hadi jirani na lango la Bournemouth kabla ya kutoa pasi maridadi kwa mfungaji. Hii inakuwa mara ya pili ndani ya mechi tatu za mwisho za Premier League kwa Pogba kutajwa kama nyota wa mchezo (Man of The Match). Ya kwanza ilikuwa dhidi ya Manchester City. Bournemouth (4-4-1-1):  Begovic 5.5; Francis 6, S Cook 5.5, Ake 7, Daniels 5..5; Fraser 6, L Cook 6.5, Surman 6 (Gosling 75, 6), Ibe 5.5 (Mousset 56, 6); King 5 (Defoe 82); W...

Mei 9 Mugabe Kujieleza Mbele Ya Bunge Kuhusu Kutoweka Kwa Almasi Zenye Thamani Ya Dola 15 Bilioni.

Akiyekuwa rais wa Zimbabwe, Robert Mugabe, ametakiwa kufika mbele ya bunge la nchi hiyo mnamo Mei 9 kujieleza kuhusu “kutoweka kwa almasi zenye thamani ya dola bilioni 15,” mbunge mmoja amesema. Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge inayohusika na maswala ya Madini na Nishati Temba Mliswa, amenukuliwa na gazeti la Herald akisema wamepanga Mei 9 kama tarehe ambapo Mugabe atatakiwa kutoa ushahidi. “Kamati hiyo ilikutana leo [Alhamisi] na iliamua kumwalika rais wa zamani Robert Mugabe kwa kamati yetu ili kujieleza kuhusu kupoteza kwa almasi zenye thamani ya bilioni 15,” ameongeza. Mugabe, ambaye alitawala Zimbabwe tangu nchi hiyo kupata uhuru wake mwaka 1980, alilazimika kujiuzulu mnamo mwezi Novemba mwaka 2017chini ya shinikizo kutoka kwa jeshi, maandamano na chama chake, Zanu-PF. Robert Mugabe ameiacha Zimbabwe katika hali ngumu kwa wananchi wake bila kusahau mgogoro wa kiuchumi unaoendelea. Wabunge wanataka kumwuliza kuhusu maneno aliyotamka mwaka 2016, ambapo alielezea mas...

TRA yawakumbusha wafanya biashara kutumiashine za EFD

Maya Magimba Afisa Msaidizi wa Huduma kwa mlipa Kodi kutoka Mamlaka ya Mapato (TRA)akitoa mada katika moja mwaka jana. Mamlaka ya Mapato Tanzania imeendelea kusisitiza  umma wa Watanzania na  wafanyabiashara kwa ujumla kutumiashine za EFD,huku ikisisitiza kuwa Mtu  binafsi awe mkazi au si mkazi anatakiwa kutembelea ofisi ya TRA ya mkoa  au wilaya na kujaza fomu ya maombi ya Namba ya Utambulisho wa Mlipakodi  (TIN). Mkuu wa Wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam Felix Lyaniva (mwenye sharti la mikono mirefu),akikata utepe katika mfao wa cheti ikiwa ni kuashiria kuanza kwa tukio la utoaji vyeti vya kutambua viwanda vidog vidogo 300 jijini.Vyeti hivyo vimetolewa na Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogo vidogo(SIDO). Hayo yamesemwa na Maya Magimba ambaye ni Afisa huduma kwa mlipakodi  wakati Shirika la kuhudumia Viwanda Vidogo vidogo(SIDO),likikabidhi  vyeti vya kutambua viwanda vidogo vidogo na vya kati kwa wam...