Na Emmanuel Richard Makundi
Nchi ya Urusi imesema ni lazima Serikali ya Iran ihusishwe kwenye
mazungumzo ya kusaka aamani ya Syria kama kiungo muhimu na mshirika wa
karibu wa utawala wa rais Bashar al-Assad.
Waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani, John Kerry (kushoto) akiteta na mwenzake wa Urusi, Sergei Lavrov (kulia) Photograph: Sergei Ilnitsky/EPA
Kauli ya Urusi inamaanisha kupuuzilia mbali maombi ya baadhi ya mataifa
ya magharibi ambayo yametaka kujumuishwa kwenye mkutano wa kimataifa wa
mjini Geneva, mkutano unaolenga kusaka amani ya kudumu nchini Syria.
Lakini kauli ya sasa ya Urusi kutaka nchi ya Iran nayo iingie kwenye
mazungumzo ya kusaidia kupatikana kwa amani ya kudumu nchini Syria
imekosolewa na nchi za magharibi ambazo zinaiona Iran kama mfadhili mkuu
wa silaha kwa wapiganaji wa Hezbollah wanaousaidia utawala wa Assad.
Hapo jana waziri wa mambo ya kigeni wa Urusi Sergei Lavrov amesisitiza
nchi yake kutuma silaha zaidi za kijeshi kwa utawala wa Syria, silaha
ambazo ni maalumu kwaajili ya kulinda anga la nchi hiyo.
Mpango huo wa Syria tayari umeibusha mgawanyiko kati yake na washirika
wanaotaka amani nchini Syria ambapo wamekosoa hatua hiyo wakisema
inalenga kuuimarisha utawala wa rais Assad.
Comments